Unene wa kupindukia unaleta saratani

Haki miliki ya picha .
Image caption Wanawake wanene kupindukia kwenye hatari ya saratani ya kizazi

Unene wa kupindukia umehusishwa na ongezeko la idadi ya wanawake wanaopatikana na saratani ya kizazi. Hii ni kwa mujibu wa Taasisi ya utafiti wa Saratani Uingereza.

Wanawake 19 kati ya laki moja waligunduliwa kuwa na Saratani hii nchini Uingereza mwaka wa 2013, ikilinganishwa wanawake 19 kati ya laki moja katika miaka ya tisini.Watafiti wamekiri kwamba kunenepa kupindukia kunaweza kuleta saratani.

Image caption Wanawake wanene kupindukia

Hata hivyo wamesema utafiti zaidi unahitajika. Nchini Uingereza wanawake 9,000 hugunduliwa na saratani ya kizazi kila mwaka huku 2000 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Watafiti wanasema matibabu yake yameimarika na kwamba wagonjwa wengi wanapona.Kwa mujibu wa Profesa Jonathan Lederman wa Taasisi ya Saratani Uingereza, siyo kwamba unene unasababisha saratani lakini unahatarisha kupata ugonjwa wenyewe.

Baadhi ya mambo mengine yanayoweza kuhatarisha kupata saratani ni pamoja na kutofanya mazoezi, umri, chakula na maumbile.