Jinsi ya kushiriki

Shindano la Faidika na BBC limefikia tamati kwa mwaka 2009, Jane Mweni ndiye mshindi. Kwa vijana wenye shauku, jiandaeni kwa maelezo zaidi ya 2010.

Unaweza kutuma maombi yako kwa njia ya posta, au kuwasilisha wewe mweyewe, katika ofisi zetu za kikanda. Vilevile unaweza kutuma maombi yako kwa anuani pepe hii: faidika@bbc.co.uk

Image caption Majaji wa Faidika

Kama unatuma maombi yako kwa njia ya posta hakikisha unatuma kwenye ofisi zetu katika nchi uliyoko.

Anuani zetu ni kama ifuatavyo ukianza na Faidika na BBC:

Kenya:

Faidika na BBC 2010, 5th Floor, Longonot Place, Kijabe Street, PO Box 58621, Nairobi

Tanzania:

Faidika na BBC 2010, PPF Building, 8th Floor, Samora Avenue and Morogoro Road, P.O Box 79545, Dar es Salaam

Uganda:

Faidika na BBC 2010, 1A, Ruth Towers, Plot 15A, Clement Hill Road, PO Box 7620, Kampala

Burundi:

Faidika na BBC 2010, Building Maison de la Bible, Avenue de la Mission, 2eme Etage, En face de PAR, Bujumbura BP 6790

Rwanda:

Faidika na BBC 2010, PO Box 2790, Kigali

DR Congo:

Faidika na BBC, Redio Maendeleo P.O. Box 3133 Bukavu République Démocratique du Congo

Vile vile unaweza kutumia anwani hii: BBC Kinshasa 20 Avenue de la Paix, Galerie Albert, 6eme Niveau Appartement, Kinshasa.

Mwanzo wa kupokea michanganuo ni tarehe mosi Septemba 2010, wakati muda wa mwisho wa kutuma michanganuo ni tarehe tatu Oktoba mwaka 2010.

Washindi watano, mmoja kutoka kila nchi zilizoshiriki, watapambana kuwania nafasi ya kwanza.

Fainali hiyo itatangazwa moja kwa moja kupitia matangazo ya jioni ya BBC, Dira ya Dunia, na vilevile katika mtandao kupitia bbcswahili.com. Jopo la majaji litaundwa na wafanyabiashara vijana kutoka Afrika Mashariki na Kati.