Ashura Kisesa, mshindi wa 2008

Mwaka wa elfu mbili na nane, Ashura Kisesa kutoka Rwanda ndiye aliyeibuka mshindi katika shindano la faidika na BBC.

Image caption Ashura Kisesa, mshindi wa pili wa Faidika

Majaji walifurahishwa sana na wazo la ubunifu wake wa kutengeneza vifaa vya kawaida vya bafuni.

Mradi huu haukuwa wa kumnufaisha yeye binafsi, bali ilikuwa ni mpango ambao utakuwa wenye manufaa kwa jamii nzima.

Mradi huo ulikuwa wakutumika kama mahala pa watu kwenda kuoga kwa maji masafi katika mazingira safi kwa malipo yaliyo nafuu.

Haikuwa rahisi kwa bi Kisesa kuutekeleza mradi wake huo kwani alikabiliwa na changamoto kutoka serikalini, wakati wa kusajili biashara hiyo ili kupata leseni ifaayo kwa mradi huo.

Swala hili lilimpotezea sana Ashura wakati muhimu lakini halikumvunja moyo.

Mwishowe aliweza kufanikiwa kuanzisha biashara ambayo imekuwa na kunawiri na ambayo imenufaisha jamii yote na kupokelewa vyema na watu wote.

Katika mahojiano haya Ashura anaeleza safari ya mafanikio yake ya biashara na msimo wa biashara yake kwa sasa