Jane Mueni, mshindi wa 2009

Katika mwaka elfu mbili na tisa, Jane Mueni kutoka Kenya ndiye aliyeebuka mshindi wa shindano la faidika na BBC.

Image caption Jane Mueni

Jane Mueni alishinda tuzo ya dola elfu tano, kwa pendekezo lake la kuzoa taka mjini Mombasa.

Wazo lake lililetwa na jinsi jamii ya mitaa ya mabanda inayoishi karibu na makazi yake ilikuwa ikikumbwa na tatizo la kuweka takataka vizuri

Aligadhabishwa sana na jinsi wakaazi hao wa mita ya mabanda walikuwa wakiishi katika mazingira yaliyokuwa yamejaa taka kila pahali. Hali hii ni tata na ya hatari kwa waakazi hao.

Alipendekeza mswada wakuweko na huduma ya usimamizi wa kuzoa takataka ambao ungeliwagharimu dola moja tu ya Marekani kwa kila nyumba.

Alinuia kuajiri vijana hamsini hivi kutoka mtaa huo wa mabanda , huku akikodisha gari ambalo lingetumika kuzoa taka hizo pamoja na kununua mifuko ya kuzoa taka na kuizungusha kwa kila nyumba.

Baada ya ushindi wake, Bi Mueni alialikwa kuhutubia kongomano la vijana la Commonwealth youth forum, nchini Trinidad and Tobago, wakati wa mkutano wa wakuu wa serikali wa Commonwealth Heads of Government Meeting (CHOGM)

Aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzake watano.