Shughuli za Kimasomaso

Kama ilivyokuwa katika awamu ya kwanza, Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilitoa vipindi kila wiki, iliyojumuisha simulizi na majadiliano, na kupeperushwa hewani kwa takriban wasikilizaji milioni 10 katika Afrika ya Mashariki.

Utafiti unaonyesha kwamba idadi hii iliongezeka kwa ajili ya kipindi cha Kimasomaso kwenda hewani na sasa inafikia millioni 16.

Kimasomaso kinatayarishwa kila wiki na kikundi cha watu watatu – chini ya usimamizi wa Mkurugenzi kuu wa BBC World Service Trust, Joerg Stalhut pamoja na Mhariri Mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akiwa London.

Katika kiwango cha maandalizi, watayarishaji kila mara huwa waangalifu kwa kujadili na kubadilishana maoni yao chini ya uongozi kutoka kwa msimamizi wa mradi akiwa London. Jambo la muhimu ni kuhakikisha ujumbe unaotolewa katika vipindi ni sanifu na kweli, na usiopendela au kumtuhumu mtu yeyote. Watayarishaji wanahakikisha kuwa kipindi hakiwadhalilishi wala kuhubiriwa vijana.

Msimamo muhimu wa Kimasomaso ni kuwawezesha vijana kufanya uamuzi wao binafsi kuhusu tabia zao baada ya kupokea ujumbe sanifu na madhubuti kuhusu jinsia na afya ya uzazi, pamoja na haki walizo nazo kisheria.

Kwa vile idhaa ya Kiswahili ya BBC hutangazia eneo zima linalozungumza Kiswahili katika afrika ya mashariki, ni muhimu kusikiliza michango kutoka sehemu zote katika eneo hili - Tanzania, Kenya, Uganda, DRC, Rwanda na Burundi, sehemu za mashambani vilevile miji na majiji.

Kipindi hupeperushwa mara tatu kwa wiki ( Jumamosi jioni saa 12 na Jumapili asubuhi (saa 12) na jioni (saa moja unusu) unaweza pia kusikiliza kupitia tovuti katika BBCSwahili.com.