Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Mgombea wa Republican Donald Trump amemshinda Hillary Clinton wa Democratic katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
  2. Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza
  3. Trump amepata kura 278 za wajumbe, Bi Clinton akiwa na 218
  4. Trump alishinda majimbo mengi yaliyokuwa yanashindaniwa

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Obama ampongeza Trump, amwalika White House

Rais Obama amempigia simu Donald Trump kumpongeza kwa ushindi uchaguzi wa urais ambapo pia amemwalika ikulu ya White House mnamo Alhamisi wajadiliane kuhusu shughuli ya mpito.

Obama pia amempigia Hillary Clinton na kumpongeza kutokana na alivyofanya kampeni.

Rais Obama atatoa taarifa zaidi Jumatano kutoka White House kujadili matokeo ya uchaguzi na hatua ambazo tunaweza kuchukua kama taifa kuungana tena pamoja baada ya kipindi cha uchaguzi huu uliokuwa na ushindani mkali", katibu wa ikulu amesema kupitia taarifa.

Taarifa kamili hii hapa:

Obama
White House

Wafuasi wa Trump washerehekea

Wafuasi wa Donald Trump wamekuwa wakisherehekea maeneo mbalimbali Marekani.

Hizi hapa ni baadhi ya picha:

Trump
EPA
Trump
Reuters
Trump
Reuters
Trump
Reuters

Putin atuma pongezi kwa Donald Trump

 Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin ametuma ujumbe wa telegramu kumpongeza Donald Trump kwa kushinda urais Marekani.

Amesema ni matumaini yake kwamba uhusiano kati ya Urusi na Marekani "utaondolewa kutoka hali ya mzozo".

Bw Trump alimsifu Bw Putin wakati wa kampeni, hatua iliyomfanya kushutumiwa na mgombea wa Democratic Hillary Clinton na wakuu wengine wa Democratic.

Soma zaidi hapa: Trump asema Putin 'ni kiongozi bora kuliko Obama'

EU yampongeza Trump na kumpa mwaliko

Wakuu wa Umoja wa Ulaya  Donald Tusk na Jean-Claude Juncker wameandika barua kumpongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump na kusisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na EU.

Wamempa mwaliko wa kuzuru Ulaya.

Waziri mkuu wa Uingereza ampongeza Trump

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amempongeza Trump kufuatia ushindi wake uchaguzi wa urais Marekani.

Amesema Marekani na Uingereza zina uhusiano maalum na wa muda mrefu na ambao msingi wake ni "uhuru, demokrasia na ujasiriamali."

Ameeleza matumaini yake kwamba Marekani na Uingereza zitasalia kuwa washirika wakuu.

"Nasubiri kufanya kazi na Rais mteule Donald Trump," amesema kupitia taarifa.

Trump
Reuters

Museveni, Kenyatta, Kagame wampongeza Donald Trump

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amejiunga na viongozi mbalimbali duniani wanaompongeza Donald Trump kwa kushinda urais Marekani.

Bw Museveni, kupitia ujumbe kwenye Twitter, amesema anasubiri kufanya kazi na Trump kama alivyofanya kazi na marais wengine waliomtangulia.

Wengine waliompongeza ni Dkt John Magufuli wa Tanzania, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Ali Bongo wa Gabon, Rais Abdul Fattah al-Sisi wa Misri, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Dkt Riek Machar pia amempongeza Bw Trump na kueleza matumaini kwamba ushindi wake utakuwa "mwisho wa watawala wa kiimla Afrika".

I congratulate @realDonaldTrump upon his election as USA president. I look forward to working with him like I've done with his predecessors.

Congratulations to @realDonaldTrump for a well earned victory.Looking fwd to continued good relationship w/ United States&new administration

Ni vigumu kujua mshindi majimbo manne

ABC News wanasema itakuwa vigumu kufanya makadirio zaidi ya matokeo ya uchaguzi katika majimbo yaliyosalia Marekani.

Wamesema majimbo ya New Hampshire, Arizona, Michigan na Minnesota ushindani ni mkali sana hivyo itakuwa vigumu kukadiria.

Trump tayari ameshinda.

Korea Kusini 'kudumisha uhusiano na Trump'

Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Yun Byung-se amesema anaamini Donald Trump ataendeleza msimamo wa sasa wa Marekani wa kutoivumilia Korea Kaskazini.

"Trump ameashiria kwamba tatizo kubwa linalokabili dunia ni silaha za nyuklia na wanachama wa kundi lake la wataalamu wa usalama wa taifa wana msimamo huo ambao unahusisha kuishinikiza vikali Korea Kaskazini," Yun amesema, akilihutubia bunge.

Waziri mkuu wa Singapore asema Trump amerudia Brexit

Waziri mkuu wa Singapore, mshirika mkuu wa Marekani barani Asia, amempongeza Donald Trump na anasema nchi yake itafanya kazi naye.

Lee Hsien Loong amesema: "Sawa na Brexit mwezi Juni, ushindi wa Bw Trump ni mtindo unaofanyika katika mataifa yaliyoendelea - kuonesha kusikitishwa kwa watu na jinsi mambo yalivyo."

Bw Trump majuzi alitaja Singapore, pamoja na China na India, kama nchi za bara Asia 'zinazoiba' nafasi za kazi kutoka Marekani.

Modi ampongeza Trump, afurahia 'urafiki'

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amempongeza Donald Trump kupitia msururu wa ujumbe kwenye Twitter.

Amesema anafurahia urafiki ambao Bw Trump ameonyesha kwa India wakati wa kampeni.  

We appreciate the friendship you have articulated towards India during your campaign, @realDonaldTrump.

Kiongozi wa EU asikitishwa na ushindi wa Trump

Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya Martin Schulz amesema ushindi wa Donald Trump ni "kura ya uasi" ambayo inafanana na Brexit (kura ya Waingereza kujitoa EU).

Ameambia redio ya Europe 1 kwamba ameshangazwa na kusikitishwa na kwamba anatarajia iwe vigumu zaidi kufanya kazi na utawala wa Bw Trump kuliko utawala wa Rais Obama.

Amemtaka Bw Trump "aheshimu maadili muhimu na uhuru wa mataifa."

Kiongozi wa zamani wa Ku Klux Klan ampongeza Trump

  David Duke, kiongozi wa zamani wa kundi la Ku Klux Klan, amempongeza Trump kupitia Twitter na pia akawapongeza "watu wetu" waliompigia kura.

Mambo ambayo Trump yakuyazungumzia

Hakuzungumza kuhusu ukuta aliosema atajenga katika mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji.

Aidha, hakuzungumzia vitisho vyake kwamba atamfunga jela  Hillary Clinton, na pia kwamba atahakikisha Waislamu wanakaguliwa sana kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

Ukurasa wa kwanza wa gazeti la New York Times

Gazeti la New York Times ambalo lilikuwa linamuunga mkono Bi Clinton.

Donald Trump
NYT

Trump: "Nitakuwa rais wa kila Mmarekani'

Akihutubu baada ya ushindi, Trump amesema: "Naahidi kila raia wa taifa hili letu kwamba nitakuwa rais wa kila Mmarekani. Na hilo ni muhimu sana kwangu.

"Kwenu ambao mliamua kutoniunga mkono siku za nyuma, na kulikuwa na watu kadha, ninaomba ushauri wanu na nitamuomba tusaidiane ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kuunganisha taifa hili letu tukufu."

Trump ashinda jimbo la Alaska

Donald Trump ameshinda jimbo la Alaska na kuchukua kura zote tatu za wajumbe kutoka jimbo hilo, kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Sasa ana wajumbe 278 naye Bi Clinton kura 218.

Mgombea huhitaji kura 270 kushinda.

Nkurunziza ampongeza Trump

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ni miongoni mwa viongozi waliompongeza Donald Trump kupitia Twitter. Amesema ushindi wa Trump ni ushindi wa Wamarekani wote.

Mr. @realDonaldTrump, on behalf of the people of Burundi, we warmly congratulate you. Your Victory is the Victory of all Americans.

Magufuli ampongeza Trump kwa ushindi Marekani

Rais wa Tanzania John Magufuli ameandika ujumbe kwenye Twitter akimpongeza rais mteule wa Marekani.

Ameahidi kwamba Watanzania wataendeleza urafiki na Marekani.

Congratulation President-Elect and people of America for a democratic election,I assure and people of Tanzania for a continued friendship.

Trump ashinda jimbo la Wisconsin

Trump ameshinda jimbo la Wisconsin na kujishindia kura 10 za wajumbe. Hilo limemuwezesha kufikisha kura 275 za wajumbe, Clinton akiwa na kura 218.

Mshindi alihitaji kura 270.

Trump Clinton
BBC

Trump ashinda jimbo la Pennsylvania

Makadirio ya ABC News yanaonesha Trump ameshinda Pennsylvania. Jimbo hilo lina kura 20 za wajumbe. Sasa Trump ana kura 265 za wajumbe na Clinton kura 218. Mshindi alihitajiwa kupata kura 270 za wajumbe.

Habari za hivi pundeTrump: Asanteni sana

Trump amepanda jukwaani Manhattan, New York. Amewashukuru wafuasi wake na kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton "kuwapongeza".

Aidha, amesema mwenyewe amempongeza Bi Clinton.

  "Hillary amefanya kazi kwa bidii sana na kwa muda mrefu sana na twafaa kumshukuru kwa alivyoitumikia nchi yetu," Bw Trump amesema.

"Sasa ni wakati wa Marekani kuponya vidonda vya mgawanyiko."

Habari za hivi pundeMike Pence, makamu wa rais mteule jukwaani

  Mike Pence, mgombea mwenza wa Donald Trump, na mkewe Karen, wamejitokeza na kupanda jukwaani mkutano wa Trump wa kusherehekea ushindi jimbo la Manhattan.  

Shangwe kambi ya Trump

Shangwe, nderemo na vifijo zimetanda miongoni mwa wafuasi wa Donald Trump.

Habari za hivi pundeClinton akubali kushindwa

  CNN na NBC wameripoti kwamba mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amempigia simu Donald Trump na kukubali kushindwa.

Habari za hivi pundeMaafisa wa Clinton wasema ni mapema mno

Mwenyekiti wa kampeni wa Hillary Clinton John Podesta amesema bado ni mapema mno na maafisa wa kampeni wa Clinton hawawezi kusema lolote kwa sasa.

"Bado wanahesabu kura na kila kura ina umuhimu ... majimbo kadha kura zimekaribiana sana kwa hivyo hatutasema mengine zaidi leo.

"Kila mtu anafaa kwenda nyumbani, alale. Tutasema mengi kesho."

Habari za hivi pundeTrump na Clinton wagawana kura Maine

ABC News wanakadiria kwamba kura tatu za wajumbe kati ya nne jimbo la Maine zitamwendea Bi Clinton.

Moja itachukuliwa na Trump.

Jimbo hilo limekuwa likiunga mkono Democratic. Mwaka 2008, Obama alikuwa mbele kwa asilimia 17. Maine na Nebraska ndiyo majimbo pekee ambapo wagombea wanaweza kugawana kura za wajumbe.

Majonzi kambi ya Clinton, shangwe kwa Trump

Wafuasi wa wagombea wakuu wa urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamepokea matokeo yanayoendelea kutangazwa kwa hisia tofauti mjini New York.  

Majonzi kwa Clinton, shangwe kwa Trump

Habari za hivi pundeMasikitiko yakumba kambi ya Clinton

Timu ya Trump ilitaraji kwamba mgombea wao angeshinda uchaguzi kama jana lakini matokeo ya uchaguzi yamewakosoa. 

 Mwandishi wa BBC Chris Gibson amekuwa akizungumza na wafuasi wa Clinton katika mkutano wake huko New York,akiwemo mfuasi mmoja ambaye alidhani kwamba matokeo hayo yangemfanya 'atapike'.

Masikitiko yakumba kambi ya Clinton mjini New York
ap
Masikitiko yakumba kambi ya Clinton mjini New York

Kufuatilia matokeo ya uchaguzi wa Marekani, Nairobi

Maafisa wa ubalozi wa Marekani, raia wa Marekani pamoja na wanahabari kadha walioalikwa, wamekuwa wakifuatilia matokeo ya uchaguzi ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.

Hivi ndivyo hali ilivyo:

Matokeo ubalozi
BBC
Matokeo ubalozi wa Marekani
BBC
Maafisa ubalozi Marekani
BBC

Mashabiki wa Trump wafurahia matokeo

"Umekuwa usiku mwema kwa mashabiki wa Donald Trump ,usiku mwema kwa raia wa Marekani na usiku mwema zaidi kwa walimwengu,Curtis Ellis mshauri mwandamizi wa timu ya kampeni za Trump .

Mashabiki wa Trump wakisheherekea matokeo ya uchaguzi
AFP
Mashabiki wa Trump wakisheherekea matokeo ya uchaguzi

Obama: "Jua lazima litachomoza asubuhi"

Kwenye ujumbe wa video, Ras Obama amesifu demokrasia bila kujali nani atashinda usiku huu (Marekani bado ni usiku).

Amesema bila kujali kitakachotokea, "Jua lazima litachomoza asubuhi."

Ameandika kwenye Twitter na kuwashauri wapiga kura "kutazamana sio tu kama wafuasi wa Democratic au Republican bali kama Wamarekani".

Obama
AFP

Trump yuko wapi kwa sasa?

Donald Trump ameondoka Trump na kuelekea hoteli ya Hilton Midtown ambapo anatarajiwa kuandaa mkutano wa ushindi

Jeff DeWitt, mkuu wa fedha jimbo la Arizona, amekuwa na Bw Trump wakifuatilia matokeo ya uchaguzi.

Amepakia picha ya Trump akimfunga tai mwanawe, na nyingine ya Trump na mgombea mwenza wake Mike Pence wakifuatilia matokeo.

Tazama:

An honor to have a front row seat in working hard to elect the next President and Vice President of the USA,… twitter.com/i/web/status/7…

Touching campaign moment as @realDonaldTrump takes time away from watching election returns to tie his son's tie.… twitter.com/i/web/status/7…

Trump
‏@JeffDeWitAZ / Twitter

Wamarekani walivyopokea ushindi wa Trump Florida

Hivi ndivyo Wamarekani walivyopokea matokeo ya uchaguzi mjini Florida

Hivi ndivyo Wamarekani walivyopokea matokeo ya uchaguzi mjini Florida
Twitter
Hivi ndivyo Wamarekani walivyopokea matokeo ya uchaguzi mjini Florida

Habari za hivi pundeClinton ashinda jimbo la Nevada

Hillary Clinton ameshinda uchaguzi wa urais jimbo la Nevada, ambapo amejizolea kura 6 za wajumbe. Sasa ana kura 215 naye Trump 244. Mshindi anahitaji kura 270.

Nevada
BBC

Mambo yalivyobadilika kwa Trump na Clinton

Wengi wameanza kujadili uwezekano wa Trump kuibuka mshindi. New York Time, gazeti lililokuwa linamuunga mkono Hillary Clinton, limechapisha mchoro wa jinsi matarajio ya mshindi wa urais yalivyobadilika.

Nate Silver, anayeandika blogu ya FiveThirtyEight (538 ni idadi ya kura za wajumbe) amesema pia kuna uwezekano wa Donald Trump kushinda urais.

Silver anafahamika kwa kuweza kutabiri matokeo katika majimbo yote 50 mwaka  2012.

Tazama mchoro hapa chini:

Uwezekano wa Trump na Clinton kushinda kwa mujibu wa New York Times
Other
Uwezekano wa Trump na Clinton kushinda kwa mujibu wa New York Times

Itakuwaje wagombea wakitoshana nguvu?

Iwapo wagombea wote wawili watatoshana nguvu kwa kura za wajumbe, kila mmoja apate kura 270, basi Bunge la Wawakilishi ndilo litakaloamua nani atakuwa rais.

Here's a fun map. What if it's a tie? Then the US House of Representatives picks the president

Here's a fun map. What if it's a tie? Then the US House of Representatives picks the president

Habari za hivi pundeClinton ana 'njia moja pekee ya kushinda'

Hillary Clinton sasa atahitajika kushinda majimbo ya Pennsylvania, Michigan na Wisconsin iwapo atashinda urais kulingana na Norm Ornstein.

 "Ana njia moja ya kupata ushindi huku Trump akiwa na njia nyingi''.

Mwandishi wa BBC wa Amerika Kaskazini Anthony Zurcher pia anakubaliana na Ornstein kuhusu umuhimu wa Michigan na Wisconsin.

Clinton is edging closer in Michigan, but a win there won't matter if she loses Wisconsin, Arizona and New Hampshire

Clinton is edging closer in Michigan, but a win there won't matter if she loses Wisconsin, Arizona and New Hampshire

Habari za hivi pundeTrump ajipatia kura 16 kutoka Georgia

Donald Trump ameshinda jimbo la Georgia kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Jimbo hilo lina kura 16 za wajumbe. Sasa Trump ana kura 244 naye Clinton 209. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

Habari za hivi pundeTrump ashinda jimbo la Iowa

Donald Trump ameshinda jimbo la Iowa, kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Amejishindia kura 6 za wajumbe. Sasa ana 228 naye Clinton 209. Mshindi anahitaji kura 270.

Habari za hivi pundeClinton ashinda jimbo la Washington

Hillary Clinton ameshinda jimbo la Washington kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Jimbo hilo lina kura 12 za wajumbe. Sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 209 za wajumbe. Mshindi anahitaji kura 270.