Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Donald Trump ameapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani
  2. Trump amechukua hatamu kutoka kwa Rais Barack Obama saa mbili usiku Afrika Mashariki. Atakula kiapo muda mfupi kabla ya saa mbili
  3. Wafuasi wake walikusanyika kwa wingi barabara za Washington.
  4. Jumamosi kunatarajiwa maandamano ya kupinga utawala wake

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Maandamano yafanyika kote Marekani

 Maandamano ya kumpinga Trump yamefanyika kote nchini Marekani

Huko San Francisco, waandamanaji waliunda minyororo ya watu kwenye daraja la Golden Gate.
Getty Images
Huko Seattle, wanafunzi waliandamana barabarani .
Reuters
Waandamanaji walibeba mabango Los Angeles
Getty Images

Gari lachomwa Washington

Gari ambalo lilihariwa mapema na waandamanaji sasa limechomwa moto Washington.

Kwa sasa wazima moto wanauzima moto huo. Moto umewashwa sehemu tofauti kote mjini humo wakati Rais Trump anaelekea Ikulu ya White House

Rais Trump na mkewe watembea kwa miguu

Rais mpya wa Marekani Donald Trump na mkewe Melanie wanatembea kwa miguu wakielekea kazi yao mapywa katika barabara ya Pennsylvania . 

 Kama ilivyo ada wakati wa kuapishwa kwa marais nchini Marekani, hutembea katika barabara hiyo wakiwa na mwana wao Barron kutoka katika gari la the Beast.

Donald Trump mkewe Melnaie na mwana wao barron wakitembea katika barabara ya Pennsylvania
BBC
Donald Trump mkewe Melnaie na mwana wao barron wakitembea katika barabara ya Pennsylvania

Msafara wa Trump waelekea Ikulu ya Whitehouse

Msafara wa rais Donald Trump's presidential motorcade unaelekea katika ikulu ya rais ukishangiliwa na idadi kubwa ya wafuasi wake waliosimama kandakando ya barabara.

Trump yuko ndani ya gari lake la The Beast.

Msafara wa Donald Trump
BBC
Msafara wa Donald Trump
Gari la The beast
BBC
Gari la The beast

Maandamano ya kumpinga Trump yafanyika duniani

Maafisa wa polisi mjini Washington DC wameambia BBC kwamba takriban waandamanji 95 wanaopinga kuapishwa kwa Donald Trump wamekamatwa kufikia sasa.

Maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa lakini hawana majeraha mabaya.

Maafisa wote wawili wamesafrishwa katika eneo la matibabu ,lakini afisa anayezungumza na vyombo vya habari hajui ni wapi. 

Katika mji mkuu wa Uhispania Madrid, waandamanaji walibeba mabango wakimtaja barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.

Katika mji mkuu wa Peru ,Lima ,waandamanaji walimshutumu msimamo wa Trump kuhusu haki za wanawake.

 Mjini Hong Kong , mwanadamanji mmoja alijifunga kwa nyororo katika lango kuu la ubalozi wa Marekani lakini akaondolewa na polisi.

takriban waandamanji 95 wanaopinga kuapishwa kwa Donald Trump wamekamatwa
Getty Images
Takriban waandamanji 95 wanaopinga kuapishwa kwa Donald Trump wamekamatwa
Katika mji mkuu wa Uhispania Madrid, waandamanaji walibeba mabango wakimtaja barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.
Reuters
Katika mji mkuu wa Uhispania Madrid, waandamanaji walibeba mabango wakimtaja barrack Obama kama 'matumaini na Donald Trump ''Chuki.
Katika mji mkuu wa Peru ,Lima ,waandamanaji walimshutumu msimamo wa Trump kuhusu haki za wanawake.
Getty Images
Katika mji mkuu wa Peru ,Lima ,waandamanaji walimshutumu msimamo wa Trump kuhusu haki za wanawake.
Mjini Hong Kong , mwanadamanaji mmoja alijifunga kwa nyororo katika lango kuu la ubalozi wa Marekani lakini akaondolewa na polisi.
Getty Images
Mjini Hong Kong , mwanadamanaji mmoja alijifunga kwa nyororo katika lango kuu la ubalozi wa Marekani lakini akaondolewa na polisi.

Ushauri wa Papa kwa Donald Trump

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis alisema katika ujumbe wake kwa rais mpya wa Marekani Donald Trump baada ya kuapishwa kwamba anafaa kuwahudumia masikini na aongozwe na maadili mema.

 ''Chini ya uongozi wako, naomba heshima ya Marekani iimarishwe kwa kuwaangazia masikini , wakiwa na wale wanaohitaji hudumu''. Mnamo mwezi Febnruari 2016 Trump alimuita Pope mwenye aibu baada ya kiongozi huyo wa dini kusema kuwa kujenga ukuta sio Ukristo.

Matamshi hayo yalionekana kama pingamizi ya hatua ya Trump kutka kujenga ukutaka kati ya mpaka wa Marekani na Mexico.

Kiongozi wa kanisa katoliki katika ujumbe wake kwa Donald Trump
BBC
Kiongozi wa kanisa katoliki katika ujumbe wake kwa Donald Trump

Trump amshukuru Clinton

Wengine wamelalama kwamba Trump alifaa kumtaja mpinzani wake Hillary Clinton katika hotuba yake , kufuatia hatua yake ya kuhudhuria kuapishwa kwake.

 Lakini kulingana na gazeti la Washinton Post ,wakati yeye na rais Bill Clinton walipowasili katika eneo hilo la kuapishwa kwa Trump,Trump alienda hadi katika meza ya familia ya Clinton na kumsalimia kwa mkono.  

Ahsante kwa kuhudhuria,Trump anadaiwa kumnong'onezea.

Trump amshukuru Clinton
BBC
Trump amshukuru Clinton

Trump atumia akaunti rasmi ya Twitter @POTUS

Trump hatimaye amechapisha ujumbe wake wa kwanza kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani @POTUS.

Hii ni mara ya kwanza kwa akaunti hiyo kuhamishwa rasmi kwa kuwa hakuna rais kabla ya Obama aliyekuwa na uwepo wake katika mitandao ya kijamii.

Trump hatimaye amechapisha ujumbe wake wa kwanza kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani
Twitter
Trump hatimaye amechapisha ujumbe wake wa kwanza kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani

Vifo vyaripotiwa katika mkutano wa Trump Nigeria

Polisi walirusha vitoa machozi katika mkutano nchini Nigeria ulioandaliwa kuonyesha uungaji mkono wa rais mpya wa Marekani Donald Trump.

 Kundi moja linalotaka kujitenga limesema kuwa watu 11 wamefariki lakini polisi wamekana kwamba hakuna mtu aliyefariki.

 Maandamano hayo yaliandaliwa katika jimbo la Southern River na wanaharakati ambao wanamtaka Trump kuunga mkono uanzilishi wa jimbo huru la Biafra kwa watu wa Igbo.

Maandamano katika mkutano wa Trump Nigeria
Nwokoleme Samuel
Maandamano katika mkutano wa Trump Nigeria

Trump achukua afisi na kuanza kusaini maagizo ya rais

Huku aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama akiendelea kuzungumza na wafuasi wake ,rais mpya Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais ,baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na rais Obama.

Trump atia saini maagizo rasmi Marekani

Obama awashukuru wafuasi wake

"Tulipoanza safari hii ,tulifanya hivyo kwa imani ya raia wa Marekani  uwezo wao, uwezo wetu wa kuungana na kulibadilisha taifa hili.

Tulijua kwamba mabadiliko hayakufanyika kutoka juu kwenda chini bali chini kwenda juu''.

Trump atumia akaunti binafsi ya Twitter

Badala ya kutumia akaunti yake mpya ya mtandao wa Twitter ya @POTUS ,rais mpya wa Marekani Donald Trump ametumia akaunti yake binafsi ya @DonaldTrump kuchapisha baadhi ya vipande vya hotuba yake.

Twitter
Twitter
Twitter

Sanamu ya Trump yachomwa Canada

Maandamano ya umoja dhidi ya Donald Trump yaendelea nchini Canada.

 Hii hapa picha kutoka Montreal

sanamu ya Trump yachomwa na waandamanaji Canada
Twitter
Sanamu ya Trump yachomwa na waandamanaji Canada

Kwaheri Obama

Obama na mkewe tayari wamepanda ndege ya kijeshi ambayo inawapeleka hadi katika kambi ya kijeshi ya Andrew Air base.

 Wakiwa huko watapanda ndege inayoelekea California kwa likizo.

 Huku Obama akiondoka ,alisalimiana kwa mkono na rais Donald Trump na mkewe na pia kuwashukuru walinzi wake. 

Joe Biden na mkewe watapanda treni ambayo itawapaleka nyumbani kwao Delaware ambako ni umbali wa saa mbili.

Ndege iliombeba Obama yaondoka
BBC
Ndege iliombeba Obama yaondoka

Trump: Uwe mweupe au mweusi sote ni watu wamoja

'Uwe mweusi, mweupe ama udhurungi sote hutokwa na damu nyenkundu' 

Melania akabidhiwa @FLOTUS

Melania Trump amekabidhiwa ukurasa rasmi wa mke wa rais @FLOTUS ambao umekuwa ukitumiwa na Michelle Obamap.

Michelle Obama sasa atakuwa anatumia @FLOTUS44

FLOTUS
BBC

Trump: Nitaunganisha dunia dhidi ya ugaidi

"Tutaunganisha ulimwengu dhidi ya ugaidi ,ambao tutauangamiza kabisa duniani.

Trump: 'Wakati wa maneno matupu umekwisha'

"Ni lazima tufikiri sana na kuwa na ndoto kubwa.

 Sitakubali wanasiasa amba huzungumza sana bila kuwatendea . 

 Wakati wa mazungumzo matupu umekwisha ,masaa ya kufanya vitendo yamewadia.

 Usikubali mtu akwambia kwamba haiwezi kufanyika''.

Hotuba ya Trump
BBC
Hotuba ya Trump

Trump: kuanzia leo itakuwa Marekani kwanza ,Marekani kwanza

Trump ameahidi kwamba  kazi na elimu zitapatiwa kipau mbele katika utawala wake.

"Tumeyafanya mataifa maengine kuwa tajiri,dhabiti .Moja baada ya nyengine viwanda vyetu vimeondoka 

Kutoka siku hii ya leo itakuwa Marekani  kwanza ,Marekani Kwanza

Donald Trump akitoa hotuba baada ya kuapishwa
BBC
Donald Trump akitoa hotuba baada ya kuapishwa

Tutaifanya Marekani kuwa taifa kuu tena

Pamoja, tutaifanya Marekani kuwa taifa kuu tena. Tutaifanya kuwa taifa tajiri tena. Ijionee fahari tena, tutaifanya salama tena. Na ndio, pamoja, tutaifanya Amerika kuwa taifa kuu tena.

Trump akabidhiwa @POTUS

Trump anapoendelea kuhutubu, tayari ukurasa wa rais wa Marekani kwenye Twitter umebadilishwa na kuwa wake. Ujumbe ulioandikwa na utawala wa Obama umefichwa na kuhifadhiwa.

Twitter
BBC

Hotuba ya Trump: 'Hili ni taifa lenu'

'Watu wangu',  ahsanteni.

Pamoja tutashauriana kuhusu njia tutakayopeleka Marekani na dunia kwa miaka mingi ijayo.

Trump: "Hii ni siku yenu ,hii ni sherehe yenu na hii ni Marekani taifa lenu.Watu waliosahaulika na wanawake hawatasahaulika tena.kila mtu anakusikiza sasa.

Cha muhimu leo sio chama kinachodhibiti serikali.lakini iwapo taifa letu linadhibitiwa na watu.

Tunahamisha mamlaka kutoka Washington na kuwapatia nyinyi Wamarekani.

Washington iliimarika lakini watau hawakugawana utajiri wake.

Trump akihutubu
BBC
Trump akihutubu

Habari za hivi pundeTrump aapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani

Trump aapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani na Jaji Mkuu John Roberts.

Makamu wa rais Mike Pence aapishwa

Makamu wa rais Mike Pence aapishwa

Makamu wa rais Mike Pence
BBC
Makamu wa rais Mike Pence

Hujambo na kwaheri!

Obama amesalimiana kwa mkono na jamaa wote wa familia ya Trump walioketi pamoja naye jukwaani.

Ameketi pamoja na mkewe, Michelle, na amesindikizwa na Joe Biden na mkewe, Jill.

Obama
Pool

Trump aingia Capitol Hill

Rais mteule Donald Trump na mkewe Melanie wameingia katika eneo la kuapishwa kwa Trump akiandamana na mwanajeshi mmoja.

 Michelle Obama pamoja na Jill Biden pia wamewasili.

 Wakati huohuo Hillary Clinton ameonekana akizungumza na rais wa zamani George Bush akisubiri.

Obama na Trump wakiwasili katika eneo la kuapishwa
BBC
Obama na Trump wakiwasili katika eneo la kuapishwa

Maandamano yalivyokuwa Washington

Mwandishi wa BBC Zuhura Yunus yupo Washington na alishuhudia maandamano yakifanyika nje kidogo mwa pahala ambapo Trump ataapishwa.

View more on facebook

Mwandishi wa BBC Tara McKelvey amekuwa akizungumza na watu kwenye mitaa ya Washington DC

"Si kila kitu ukipendacho kitakuwa kama unavyotaka kiwe'

Chanty Sem, raia wa Cambodia anayeishi Phoenix.
BBC
Tunatumai rais mpya ataipeleka dunia katika amani '' anasema Chanty Sem, raia wa Cambodian anayeishi Phoenix.
Raymond Garcia,
BBC
Wakati huo huo, Raymond Garcia, mhandisi mstaafu kutoka Houston, anawatembelea wajukuu zake walioko mjini Washington. Anasema hakumpigia kura Trump, lakini kwa sasa anamuunga mkono.

Trump na Obama waelekea Capitol Hill

Rais Obama na mwenzake mteule Trump wameondoka katika ikulu ya Whitehouse amoja na sasa wanaelekea katika eneo atakaloapishwa Trump.

 Mkewe Obama na Melanie Trump pia wako katika gari mbele ya viongozi hao wakielekea Capitol Hill. 

Makamu wa rais Joe Bidden na makamu wa rais mteule Mike Pence wanaelekea katika gari jingine.

Obama na Trump wakitoka katika ikulu ya Whitehouse
BBC
Obama na Trump wakitoka katika ikulu ya Whitehouse
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake mteule Mike Pence
BBC
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake mteule Mike Pence

Waandamanaji wanaompinga Trump wavunja vioo vya maduka

Hali ya wasiwasi imetanda katika maeneo ya mji mkuu wa Marekani.

Waandamanaji waliovalia nguo nyeusi wametupa mapipa ya taka barabarani na kuvunja vioo vya madirisha ya maduka. 

Walinzi walifunga eneo moja la kuingilia baada ya kuvamiwa na waandamanaji wa Black Lives Matter. 

Waandamanaji waliimba nyimbo dhidi ya Trump na kuwazuia watu kuingia katika eneo hilo la kuapihswa kwa Trump .

Lakini wafuasi wa Trump waliwapigia kelele waandamanaji hao. Wakati huohuo makamu wa rais wa zamani nchini Marekani akiwemo Dan Quayle and Dick Cheney wamefika na kuketi.

Walinzi wafunga eneo moja la kuingilia Capitol Hill ili kuwazuia waandamanaji
Twitter
Walinzi wafunga eneo moja la kuingilia Capitol Hill ili kuwazuia waandamanaji

Obama alivyoondoka afisi yake mara ya mwisho

Obama akiondoka afisi yake White House mara ya mwisho

Bintiye Muhammad Ali kushiriki maandamano ya kumpinga Trump

Maryum Ali, bintiye mchezaji ndondi wa zamani Muhammad Ali, ni miongoni mwa watu wanaofanya maandamano ya kupinga urais wa Donald Trump. Maryum Ali atajiunga na maandamano ya wanawake. 

Habari za hivi pundeHillary Clinton awasili

Hillary Clinton, mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa na Trump, amewasili kwenye majengo makuu ya Bunge la Congress katika jumba la Capitol ambapo Trump ataapishwa.

Iwapo mambo yangeenda sawa kwake, angekuwa rais wa kwanza mwanamke na angekuwa ndiye mgeni mkuu wa heshima leo. Lakini hayo yalisalia hivyo, matamanio...

Imetoka mara kadha mpinzani kushuhudia aliyemshinda akiapishwa.

Miongoni mwa waliofanya hivyo ni makamu wa marais waliokuwa wanaondoka Richard Nixon mwaka 1961 na Al Gore mwaka 2001 waliposhuhudia waliowashinda wakiapishwa.

Clinton kushuhudia Donald Trump akiapishwa Marekani

Maandalizi ya mwisho katika eneo la Capitol Hill

Wakati huohuo viti vimeanza kuwekwa katika eneo la mbele la eneo la Capitol  huku sherehe ya kuapishwa kwa rais wa 45 nchini Marekani zikitarajiwa kuanza saa chache kutoka sasa.

Wanachama wa kundi la kwaya ya Mormon Tabernicle ambao wamealikwa na Trump kumuimbia tayari wamewasili wakivalia makoti ya kuzuia mvua.

Eneo la Capitoll Hill ambapo sherehe za kuapishwa kwa Trump zitafanyika
Getty Images
Eneo la Capitoll Hill ambapo sherehe za kuapishwa kwa Trump zitafanyika
Kwaya ya wanachama wa Mormon Terbanicle
BBC
Kwaya ya wanachama wa Mormon Terbanicle

Obama kuhamia Washington

Rais Barack Obama wa Marekani ameoondoka katika ikulu ya White House lakini hatahamia mbali.

 Bwa Obama alisema siku awali kwamba familia yake itahamia mjini Washington, huku mwanawe wa kike Sasha akimaliza shule katika Elite Academy, Sidwel Friends.

 ''Kumhamisha mtu katikati ya mafunzo ni vigumu'', alisema alipokuwa akijibu maswali huko Wisconsin.

 Kwa habari zaidi:Obama kuhamia Washington DC

Rais Obama na familia yake
BBC
Rais Obama na familia yake

Trump akutana na Obama

Trump ameingia White House baada ya kuamkuana na rais anayeondoka na mkewe.

Rais huyo mteule amewapungia mkono wanajeshi wanaolinda lango la kuingia White House kabla ya kupigwa picha rasmi.

Sasa, wameingia ndani kunywa kahawa na chai.

"Nafurahi sana kuwaona. Hongera," Obama ameambia Trump na mkewe alipokuwa anawasalimia kwa mkono.

"Vyema kabisa," amejibu Trump.

The Trumps arrive at the White House to meet the Obamas on #InaugurationDay bbc.co.uk/inauguration

Trump aondoka kanisani, aelekea White House

Donald Trump na mkewe Melania wameondoka kanisani St John's na kuelekea White House.

Wanatarajia kunywa kahawa kwa pamoja na familia ya Obama, rais anayeondoka.

Wabunge 50 kususia kuapishwa kwa Trump

Trump International house
Getty Images
Wanajeshi wa jeshi la Marekani wakiwa wamesimama mbele ya Trump International Hotel, iliyopo karibu na White House

Wabunge zaidi ya 50 wa chama cha Democratic katika Bunge la Congress watasusia sherehe za kuapishwa leo kwa Trump - ukiwa ni upinzani mkubwa wa kisiasa dhidi ya rais mpya. 

 Wengi miongoni mwa watakaosusia sherehe hizo wamesema wameamua kufanya hivyo kutokana chuki inayoendelezwa baina ya Bwana Trump na mwana hararakati wa haki za kiraia na mjumbe wa congresi , John Lewis.

 Bwana Lewis, mpigania haki za kiraia aliyepata umaarufu miaka ya 1960 ambaye pia amekataa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Trump, amesema anauona ushindi wa Bwana Trump Kama usio wa kisheria kutokana na madai ya Urusi kuingilia uchaguzi. 

 Bwana Trump alijibu kwa kuseam kuwa "wote maneno tuu, maneno, maneno, maneno - hakuna vitendo wala matokeo ".

 Kiwango cha kususia sherehe za kuapishwa kwa Bwana Trump si kikubwa katika historia. Mnamo mwaka 1973, Wajumbe 80 wa baraza la Congresi walisusia kuapishwa kwa Richard Nixon.

Obama ameondoka afisi yake White House

Obama ameondoka afisi yake White House kwa mara ya mwisho kama rais. Kama ilivyo mtindo, amemwachia mrithi wake barua kwenye meza yake afisi ya rais, Oval Office. Yaliyomo hayajafichuliwa.

Ameandika hivi kwenye Twitter:

I'm still asking you to believe - not in my ability to bring about change, but in yours. I believe in change because I believe in you.

As we look forward, I want our first steps to reflect what matters most to you. Share your thoughts with me at Obama.org.

Maandamano kuhusu Trump kwa picha

Maandamano dhidi ya Trump
Getty Images
Mwanamume wa Kipalestina katika maandamano dhidi ya makazi ya Israeli tarehe 20 Januari
Waandamaji wa London waliandamana kwenye daraja la Millennium Bridge
Getty Images
Waandamanaji waliandamana kwenye daraja la Millennium Bridge jijini London pia
Umati wa watu wakiukaribisha utawala mpya mjini Kiev
Getty Images
Umati wa watu nje ya ubalozi wa Marekani mjini Kiev wakiukaribisha utawala mpya
Waandamanaji waliweka bango la ujumbe kwa Trump
Getty Images
"Jenga madaraja, sio kuta" bango lilining'inizwa kwenye daraja la - Tower Bridge