Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Makadirio ya matokeo ya uchaguzi yanaonesha Conservatives watakuwa na wabunge wengi
 2. Conservatives hata hivyo watapata wabunge 314 na kukosa wingi wa wabunge
 3. Chama cha Labour kinatarajiwa kujiongezea wabunge 34
 4. Kuna takriban wapiga kura 46.9 milioni walitarajiwa kushiriki uchaguzi

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

May kuomba idhini ya kuunda serikali Uingereza

Theresa May
PA
May amesema Uingereza inahitaji uthabiti

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atafika Kasri la Buckingham mwendo wa saa 12:30 BST (saa nane unusu adhuhuri Afrika Mashariki) kuomba idhini ya kuunda serikali, licha ya chama chake kupoteza wingi wa wabunge uchaguzini Alhamisi.

Atajaribu kuendelea kuongoza, akiwa na ufahamu kwamba chama cha Democratic Unionist Party kitaunga mkono serikali yake.

Huku kukiwa na maeneo bunge mawili ambayo matokeo yake hayajatangazwa, Conservatives wanapungukiwa na wabunge wanane kufikisha wabunge 326 wanaohitajika kuwa na wingi wa wabunge.

Kiongozi wa chama cha Labour kilicho cha pili kwa idadi ya wabunge Jeremy Corbyn amemtaka kujiuzulu na kusema chama chake kiko tayari kuongoza.

Kiongozi wa UKIP ajiuzulu

Kiongozi wa UKIP Paul Nuttall ameng'atuka kutoka kwenye wadhifa wake kama kiongozi wa chama hicho baada ya chama hicho kukosa kushinda kiti hata kimoja cha ubunge katika ucahguzi mkuu Alhamisi.

Waziri wa tano apoteza kiti uchaguzini

Waziri wa Utamaduni Rob Wilson ameshindwa katika uchaguzi eneo bunge lake la Reading Mashariki na mgombea wa chama cha Labour.

Amefikisha tano, idadi ya mawaziri walioshindwa.

Wengine ni:

 • Jane Ellison (waziri wa Hazina Kuu)
 • Ben Gummer (Waziri katika afisi ya Baraza la Mawaziri)
 • Gavin Barwell (Waziri wa Nyumba na Makao)
 • James Wharton (Waziri wa Ustawi wa Kimataifa)

Kiongozi wa zamani wa SNP ashindwa

Alex Salmond, aliyekuwa kiongozi wa chama cha SNP, ameshindwa uchaguzini jimbo la Gordon na mgombea wa chama cha Conservative.

Salmond
BBC

Bedfordshire South West: Chama cha Conservative chashikilia

Maeneo ya Bedfordshire South West: yanyakuliwa na Chama cha Conservative ambacho sasa kinashikilia, ilihali Twickenham: kimekuwa faida ya chama cha Liberal Democrat kutoka mikononi mwa Conservative

Awapiku wenzake kwa kura 32,961
BBC
Matokeo ya Bedfordshire South West, yakionyesha kunyakuliwa na Andrew Selous

Priti Patel amtetea Theresa May

Katibu wa shirika la kimataifa la maendeleo Priti Patel, ameuliza hatma ya baadaye ya waziri mkuu wa Uingereza, akisema ni "anatizama picha kubwa ya uamuzi huo, na chaguo kubwa" na ni nani anayetakiwa kusimamia hayo.

Anasema sio "sahihi kusema kuwa, hatukulenga uamuzi wa Uingereza kujiondoka kutoka kwa Jumuia ya mataifa ya Bara Ulaya", huku akiyarejelea maswala muhimu 12 ya Waziri mkuu, ilihali "wengine wanataka kuhujumua hatua hiyo ya Brexit huku chama cha Labour kikiwa hakina hasa mpango madhubuti".

Pia alitetea mipango ya Bi May ya kuitisha uchaguzi wa mapema, akisema kuwa "alieleweka" lilikuwa wazo la "kutizama yajayo na kuboresha msimamo wake".

Anasema ni kuhusu "kutizama yajayo na kuboresha msimamo wake".
BBC
Utetezi wa May kutoka kwa Priti Patel

Vijana 'wafanya eneo la kushindaniwa linyakuliwe na chama cha Labour'

BBC Radio 4 inaripoti kuwa, duru kutoka kwa chama cha Labour, zinadai kuwa watashinda viti vya Wrexham na pia kile cha Clwyd South.

Maeneo hayo yalikuwa yakilengwa na chama cha Concervative, lakini idadi kubwa ya vijana iliyojitokeza, inaaminika imesaidia kuboresha kura ya chama cha Labour.

Vijana Chipukizi
BBC
Vijana wajitokeza kwa wingi kuunga mkono chama cha leba

Nini kitafanyika sasa baada ya uchaguzi Uingereza?

Je, chama chenye wabunge wengi kitaunda serikali?

Si lazima. Chama chenye wabunge wengi baada ya kura zote kuhesabiwa maeneo yote 650, huwa kinatangazwa mshindi na kiongozi wake huwa waziri mkuu.

Lakini hili huenda lisifanyike wakati huu kwa kuwa chama kilichoshinda hakina wingi wa wabunge. Inawezekana kwa chama kilichomaliza cha pili kuunda serikali.

Soma zaidi: Nini kitafanyika sasa baada ya uchaguzi Uingereza?

Kiongozi wa UKIP: Brexit imo hatarini

Kiongozi wa UKIP Bw. Paul Nuttall amesema kuwa Bi Theresa May ameiweka Brexit kwenye hatari kubwa. Anasema tangu mwanzo hatua hiyo haikuwa sawa.

If the exit poll is true then Theresa May has put Brexit in jeopardy. I said at the start this election was wrong. Hubris.

Matokeo ya utafiti ya baada ya uchaguzi yanabashiri kuwa chama cha SNP kitapoteza viti 22

Chama cha SNP chenyewe kilitabiri kunyakuwa viti 34 huku kile cha Conservatives kikishindwa karibu kila mahali nchini Uingereza.

Fallon haamini matokeo yaliyobashiriwa ya baada ya upigaji kura

Waziri wa ulinzi nchini Uingereza Sir Michael Fallon anasisitiza kuwa ubashiri uliotolewa na vyombo vya habari vya BBC/ITV/Sky, ya matokeo ya utafiti ya baada ya upigaji kura ni ubashiri tu ambao haamini, huku akiongeza kuwa "mnamo mwaka 2015 hawakukadiria vilivyo kura zetu".

"Acha tusubiri ili tuone viti viti vitakwendaje," alisema

Hakuna atakayekuwa na wingi wa wabunge

Matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi wa BBC, ITV na Sky yanaonesha hakuna chama kitakachopata wingi wa wabunge katika Bunge la Commons.

Hakuna chama kitakachoweza kufikisha idadi ya wabunge 326.

Matokeo
BBC

Habari za hivi pundeUtafiti: Conservatives wanaongoza uchaguzi Uingereza

Matokeo ya utafiti wa pamoja wa BBC, ITV na Sky, ambao hufanyika baada ya watu kupiga kura, yanaonyesha chama cha Conservatives kitaongoza kwa kupata wabunge 314.

Hii itakuwa na maana kwamba chama hicho cha Theresa May kitakuwa kimepoteza viti 17.

Chama cha Labour kitapata wabunge 266, chama hicho cha Jeremy Corbyn kikiongeza viti 34.

Liberal Democrats watapata viti 14 nao SNP viti 34.

Chama cha Plaid kitapata viti vitatu, Greens kimoja nao UKIP wapoteze kiti chao pekee bungeni. Vyama hivyo vingine vyote vitakuwa na viti 18.

Utafiti huo hufanyika katika vituo 144 vya kupigia kura Uingereza, ambapo wapiga kura huombwa hupiga kura tena katika karatasi mwigo baada yao kuondoka vituoni kuonyesha walivyopiga kura.

Utafiti kama huo umefanikiwa kubashiri nani atashinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu mara tano awali. Miaka 2005 na 2010, utafiti huo ulikaribia sana kubashiri hata idadi ya viti ambavyo mshindi angepata.

Soma zaidi: Conservatives kuwa na wabunge wengi

Habari za hivi pundeVituo vya kupigia kura vyafungwa

Kengele katika mnara wa Big Ben imegonga saa nne usiku Uingereza (saa sita usiku Afrika Mashariki), vituo vya kupigia kura vimefungwa.

Matokeo ya utafiti kutangazwa karibuni

Matokeo ya utafiti wa pamoja wa BBC, ITV na Sky, ambao hufanyika baada ya watu kupiga kura, yanakaribia kutolewa.

Yataashiria nani huenda akashinda.

Utafiti huo hufanyika katika vituo 144vya kupigia kura Uingereza, ambapo wapiga kura huombwa hupiga kura tena katika karatasi mwigo baada yao kuondoka vituoni kuonyesha walivyopiga kura.

Utafiti kama huo umefanikiwa kubashiri nani atashinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu mara tano awali. Miaka 2005 na 2010, utafiti huo ulikaribia sana kubashiri hata idadi ya viti ambavyo mshindi angepata.

Dakika mbili kabla ya vituo vya kupigia kura vifungwe

Mwandishi wa BBC ni mmoja wa wale wanaosubiri kufungwa kwa vituo vya kupigia kura ili shughuli za kuhesabu zianze.

Here's the BBCNI green screen team, ready for the thrills (and spills) of election night.

Here's the BBCNI green screen team, ready for the thrills (and spills) of election night.

Sunderland mbioni kutaka kuwa ya kwanza kutangaza matokeo

Sunderland imekuwa kidedea kila mara katika maeneo bunge yaliyo ya kwanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu Uingereza.

Habari kutoka huko zinasema maafisa wanafukuzana na muda ili iwe bado ya kwanza kutangaza matokeo.

Ni mbio za kazi hapa
Ian Forsyth/Getty
Maofisa katika kituo cha kuhesabia kura huko Sunderland wanajizatiti vilivyo

Vituo vya kupigia kura visivyo vya kawaida Uingereza

Nchini Uingereza, kuna maeneo mengi ambayo yamegeuzwa kuwa vituo vya kupigia kura ambayo si ya kawaida. Mwanzo ni baa hii:

The Thatched House
BBC
Kuna pia kinu kilichogeuzwa kituo cha kura
BBC
Kuna pia kinu kilichogeuzwa kituo cha kura
Kituo hiki cha dobi leo ni kituo cha kupigia kura
BBC
Kituo hiki cha dobi leo ni kituo cha kupigia kura

Tunaweza kumfahamu mshindi mapema?

Kidokezo cha kwanza kuhusu nani huenda akaibuka na ushindi kitapatikana baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa, saa sita usiku Afrika Mashariki (22:00 BST), matokeo ya utafiti wa upigaji kura wa BBC/ITV/Sky yatakapochapishwa.

Katika uchaguzi uliopita na uliotangulia huo, matokeo hayo ya utafiti yalikaribia sana kubashiri matokeo kamili kwa ufasaha.

Matokeo halisi ya kwanza kama kawaida huwa ni kutoka maeneo bunge matatu Sunderland, ambayo huhesabu kura mapema.

Ili kupata wingi wa kura Bunge la Commons, chama kimoja kkinatakiwa kujishindia viti angalau 326. Mwaka 2015, ushindi wa chama cha Conservative ulithibitishwa saa 13:34 BST (saa tisa na dakika 34 alasiri).

Viongozi walivyopiga kura Uingereza

Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini Uingereza wamepiga kura katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Hapa chini ni picha za viongozi hao baada ya kupiga kura.

Jeremy Corbyn na Theresa May baada ya kupiga kura Alhamisi
EPA/PA
Jeremy Corbyn na Theresa May baada ya kupiga kura Alhamisi
Kiongozi wa Liberal Democrats Tim Farron alionekana mchangamfu licha ya mvua baada yake kupiga kura Kendal, Cumbria
AFP
Kiongozi wa Liberal Democrats Tim Farron alionekana mchangamfu licha ya mvua baada yake kupiga kura Kendal, Cumbria
Kiongozi mwenza wa chama cha Green Party Caroline Lucas na mkewe Richard Savage baada ya kupiga kura Brighton
Reuters
Kiongozi mwenza wa chama cha Green Party Caroline Lucas na mkewe Richard Savage baada ya kupiga kura Brighton
Kiongozi wa chama cha UKIP Paul Nuttall alipiga kura yake Congleton, Cheshire
Reuters
Kiongozi wa chama cha UKIP Paul Nuttall alipiga kura yake Congleton, Cheshire
Mjini Glasgow, kiongozi wa chama cha SNP Nicola Sturgeon alipiga kura katika ukumbi wa jamii
EPA
Mjini Glasgow, kiongozi wa chama cha SNP Nicola Sturgeon alipiga kura katika ukumbi wa jamii
Kiongozi wa Plaid Cymru, Leanne Wood, alipigia kura yake Penygraig
BBC
Kiongozi wa Plaid Cymru, Leanne Wood, alipigia kura yake Penygraig

Matokeo yatajulikana saa ngapi Uingereza?

Matokeo ya kwanza yataangza kutangazwa muda mfupi baada ya vituo kufungwa, mwendo wa saa sita usiku Afrika Mashariki.

Lakini inakadiriwa kwamba ili kufahamu mwelekeo kamili wa matokeo, huenda watu wakasubiri hadi mwendo wa saa kumi na mbili hivi asubuhi Afrika Mashariki! Utaweza kukesha hadi wakati huo?

Je ni wanasiasa gani wamewania mara nyingi zaidi Uingereza?

Winston Churchill anachukua nafasi ya kwanza. Aliwania katika uchaguzi 16 kwa jumla. Mara ya kwanza ikiwa mwaka wa 1900 na ya mwisho, mwaka wa 1959. Aliibuka mshindi mara 14.

Wa pili ni Charles Pelham Villiers aliyesimama katika uchaguzi 15 kati ya 1835 na 1895 na alishinda zote.

Waziri mkuu wa zamani wa Conservative Edward Heath ni mmoja wa baadhi ya wanasiasa ambao walisimama katika uchaguzi 14, lakini pamoja na TP O'Connor wa Ireland, ni yeye pekee katika kikundi hicho aliye na mafanikio ya asilimia 100.

Kutoka chama cha Leba, Gerald Kaufman na Manny Shinwell wote walisimama mara 14, na kushinda mara 12.

Vituo vya kupiga kura vitafungwa saa ngapi?

Vituo vya kupigia kura viko wazi na wapiga kura wanaendelea kupiga kura zao katika uchaguzi ulioitishwa na Theresa May.

Kuna zaidi yawagombea 2,700 wanaowania viti 533 nchini Uingereza kati ya jumla ya viti 650. Wapiga kura waliosajiliwa wanaweza kuchagua wanayemtaka kuwa mbunge wao hadi saa sita usiku saa za afrika mashariki.

Kuhesabu kura kutafanyika usiku na washindi watatangazwa mapema Ijumaa asubuhi.

Katika uchaguzi mkuu wa 2015, kulikuwa na wagombea 3209 katika majimbo yote ya Kiingereza, 493 zaidi ya wagombea wa wakati huu.

Wapiga Kura ambao waliomba kutumia njia ya Posta lakini hawakurejesha kadi zao mapema bado wanaweza kuzipeleka kwenye vituo vyao vya kupiga kura kabla ya saa ita usiku saa za Afrika Mashariki (22:00 BST).

Kulikuwa na ulinzi mkali katika kituo cha kupigia kura cha Berkshire ambapo Theresa May alipiga kura.
EPA/FACUNDO ARRIZABALAGA
Kulikuwa na ulinzi mkali katika kituo cha kupigia kura cha Berkshire ambapo Theresa May alipiga kura.

Uchaguzi mkuu : Baadhi ya takwimu muhimu

 • Milioni 46.9: Idadi ya watu walio na haki ya kupiga kura

 • Milioni 1.1: Idadi ya wapiga kura ambao wamesajiliwa tangu 2016

 • 3,304: Idadi ya wagombeaji kutoka vyama vyote

 • 974: Idadi ya wagombeaji wanawake katika uchaguzi huu

 • 326: Idadi ya viti vinavyohitajika kwa upande wowote kufanya kazi

 • 17: Idadi ya wabunge waliounga serikali mkono mwishoni mwa bunge la 2015-17

 • 97: Idadi ya viti inayohitaji chama cha Leba ili kushinda

 • 650: idadi ya majimbo nchini Uingereza

Baadhi ya Picha katika vituo vya kupigia kura

Wapiga kura kwenye foleni katika kanisa la Sacred Heart, Wimbledon, London.
Shutterstock
Wapiga kura kwenye foleni katika kanisa la Sacred Heart, Wimbledon, London.
Nyumba hii eneo la Croydon inatumika kama kituo cha kupigia kura.
Ben STANSALLBEN STANSALL/AFP/Getty Images
Nyumba hii eneo la Croydon inatumika kama kituo cha kupigia kura.
Wanandoa hawa walifika katika kituo cha kupiga kura eneo la Lisburn, Ireland ya Kaskazini, wakiwa bado wamevalia nguo za harusi yao baada ya kufunga ndoa mapema leo.
Brian Lawless/PA Wire
Wanandoa hawa walifika katika kituo cha kupiga kura eneo la Lisburn, Ireland ya Kaskazini, wakiwa bado wamevalia nguo za harusi yao baada ya kufunga ndoa mapema leo.
Wapiga kura wa Guisborough, wanajikinga mvua.
Ian Forsyth/Getty Images
Wapiga kura wa Guisborough, wanajikinga mvua.
Otto na Ava kutokaHampshire wanaelekea kupiga kura.
TWITTER/@DACHSHUNDOTTO
Otto na Ava kutoka Hampshire 'wanaelekea kupiga kura'?

Hujambo!

Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu Uchaguzi Mkuu Uingereza mwaka 2017. Wapiga kura takriban 45.9 milioni wanapiga kura kuwachagua wabunge 650.

Makazi haya ya kibinafsi Hampshire yanatumika kama kituo cha kupigia kura
Andrew Matthews/PA Wire