Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Idadi ya wapiga kura waliojitokeza ni 33.4% (6,553,858) katika maeneo bunge 267 kwa mujibu wa mwenyekiti wa IEBC
  2. Makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi yalishuhudiwa ngome za upinzani Alhamisi
  3. Matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo tofauti yanaendelea kupokelewa katika ukumbi wa Bomas
  4. Uchaguzi utarudiwa Jumamosi majimbo manne pamoja na maeneo mengine ambayo uchaguzi ulivurugika Alhamisi

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Tume ya uchaguzi IEBC yaahirisha uchaguzi wa tarehe 28 magharibi mwa Kenya

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imetangaza kuhairishwa kwa uchaguzi wa urais ambao ulitarajiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi huu katika kaunti nne magharibi mwa Kenya yaliyo kwenye ngome ya upinzani.

Kaunti hizo ni pamoja Migori, Siaya, Kisumu na Homa Bay.

Uchaguzi huo ulihairiswa kwa sababu za kiusalama maeneo hayo wakati wafuasi wa upinzani wakipinga kufanyika marudio ya uchaguzi

Katika taarifa yake Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kuwa tume imechukua hatua hiyo ili kulinda maisha ya wafanyakazi wake.

Wafula Chebukati
Getty Images/AFP

Habari za hivi pundeOdinga kutangaza hatua ya kuchukua Jumatatu

Bw Odinga amewaambia wafuasi wake Kibera, Nairobi kwamba atatangaza hatua ya kuchukua Jumatatu.

Odinga: Tutakarabati shule maeneo yaliyoharibiwa

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametembelea mtaa wa Kibera ambapo amesisitiza kwamba upinzani hautalegeza msimamo wake.

Amesema shule mbili ambazo ziliharibiwa wakati wa makabiliano ya wafuasi wake na polisi jana wakati wa uchaguzi zitakarabatiwa.

Uchaguzi mmoja, mazingira tofauti

Jana Alhamisi, uchaguzi ulikuwa mmoja lakini mazingira tofauti maeneo ambayo ni ngome ya upinzani na ngome ya serikali.

Tazama:

View more on facebook

Habari za hivi pundeMudavadi: Tunaitaka IEBC kufuta uchaguzi wa marudio

Mmoja wa viongozi wa Nasa Musalia Mudavadi ameshutumu hatua ya tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi majimbo manne magharibi mwa Kenya na kusema utafanyika kesho Jumamosi.

Bw Mudavadi ametoa wito kwa tume ya uchaguzi kufuta uchaguzi huo.

Amewashutumu polisi akisema wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na wakazi katika maeneo yanayoaminika kuwa ngome ya upinzani.

"Serikali hii haijafurahi kwamba watu wameikataa, inatumia nguvu kuwakabili wapinzani wake," amesema.

Chebukati: Matokeo yatatangazwa ngazi ya maeneo bunge

Chebukati
BBC

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema tume hiyo imepokea fomu za matokeo ya vituoni kutoka katika vituo vyote ambavyo upigaji kura ulifanyika.

Amesema wamepokea Fomu 34A jumla ya 37045.

Amesema kwa sasa wasimamizi wa uchaguzi vituoni wamekuwa wakiwasili katika kituom cha taifa cha kujumlishia matokeo ukumbi wa Bomas Nairobi ambapo uhakiki wa matokeo utafanyika.

Amesema kwa sasa maeneo bunge 15 kati ya 290 yamewasilisha matokeo na uhakiki wa matokeo ya maeneo hayo utaanza.

Mwanamume auawa kwa risasi katika maandamano Bungoma

Taarifa zinasema mwanamume mmoja amepigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wamefunga barabara ya Bungoma-Mumias katika mji wa Bungoma, magharibi mwa Kenya.

Polisi wamefyatua risasi na kurusha gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao.

Spika wa bunge la seneti Ken Lusaka amewaambia wanahabari kwamba kijana aliyepigwa risasi alikuwa akijaribu kumpokonya afisa wa polisi silaha yake. Madai yake hata hivyo hayajathibitishwa.

View more on twitter

Wasimamizi wa uchaguzi vituoni wameanza kuwasili Bomas

Tume ya uchaguzi imesema maafisa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura wameanza kuwasili katika kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo ukumbi wa Bomas, nairobi.

Maafisa hao wanafaa kuwasilisha fomu 34A (fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura) moja kwa moja hadi Bomas.

Ni fomu hizo ambazo walitakiwa kutanguliza kuzituma kwa njia ya kielektroniki na kuziweka kwenye mtandao.

View more on twitter

Chebukati: Tumepokea fomu 36,769 kufikia sasa

Chebukati
AFP/Getty

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati amesema tume hiyo kufikia sasa imepokea fomu za matokeo kutoka vituo 36,769.

Anasema idadi hiyo ni ya juu ukilinganisha na idadi ya fomu walizokuwa wamepokea kipindi sawa wakati wa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.

View more on twitter

Vijana watumia nyuki kuzuia upigaji kura Kenya

Shuguli ya kupiga kura ikiendelea katika maeneo mbalimbali siku ya Alhamisi
BBC
Shuguli ya kupiga kura ikiendelea katika maeneo mbalimbali siku ya Alhamisi

Maafisa wa polisi walikuwa na wakati mgumu kuwadhibiti vijana waliotumia nyuki kufunga kituo kimoja cha kupigia kura katika eneo bunge la Malava kakamega kaunti.

Vijana hao walibeba mzinga wa nyuki katika shule ya msingi ya Matsakha na kuwalazimu maafisa wa IEBC kuwaita maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Malava.

Wapiga kura wachache walilazimika kuondoka katika lango la kituo hicho cha kupiga kura kwa hofu ya kushambuliwa na nyuki.

Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Malava Anne Muli aliongiza operesheni ya kukabiliana na nyuki hao.

Awali maafisa wa polisi walikuwa wamewakamata baadhi ya vijana katika eneo la Matsakha na Shilongo kwa kujaribu kuharibu uchaguzi.

Vichwa vya magazeti ya Kenya

Vichwa vya magazeti ya Kenya kufuatia marejeleo ya uchaguz mkuu nchini Kenya ambao uliusiwa na upinzani

Vichwa vya magazeti ya Kenya kuhusu uchaguzi wa Kenya
BBC
Vichwa vya magazeti ya Kenya kuhusu uchaguzi wa Kenya

Chebukati: Waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 33.4

Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekadiria kwamba marejeo ya uchaguzi wa urais imefikia asilimia 33.4 .

Hiyo ikiwa ni chini kwa asilimia 8 ikilinganishwa na uchaguzi wa mwezi Agosti ikionyesha kuwa mamilioni ya Wakenya walifuata wito wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kususia uchaguzi huo.

Upigaji kura umesitishwa hadi siku ya Jumamosi katika kaunti nne ambapo wafuasi wa upinzani walizozana na maafisa wa polisi.

Gavana wa kaunti ya Kisumu aliambia BBC kwamba waandamanaji wawili uawa kutokna ana majereha ya risasi. Waandishi wanasema kuwa idadi hiyo ya waliojitokeza, kupiga kura inazua maswalai kuhusu uchagzi huo.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
BBC
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati