Huwezi kusikiliza tena

Mjadala: Profesa Baregu na Kinana

Mimi ni Hassan Mhelela, katika makala ya Wiki Hii, leo tunajikita zaidi kuangalia mwenendo wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania, kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu tarehe 31 mwezi ujao wa Oktoba.

Kujadili maswala mbali mbali ya kampeni hizo, ikiwa ni pamoja kurushiana matope, nawakutanisha Profesa Mwesiga Baregu meneja wa kampeni wa CHADEMA, na vile vile Abdulrahman Kinana meneja wa kampeni za chama tawala cha CCM. Kwanza ni Profesa Baregu, nimetaka aelezee maswala muhimu ya kampeni ya CHADEMA mwaka huu.