Huwezi kusikiliza tena

TeknoMaarifa

Kampuni ya simu ya Nokia imezindua simu mpya tatu kwa lengo la kukabiliana na upinzani wa makampuni yaliyoibuka miaka ya karibuni, Honda imeonyesha jinsi hydrogen inavyotumika kuendeshea magari kwa gharama nafuu pasipo kuchafua mazingira. Hayo anayasimulia Hassan Mhelela katika makala ya TeknoMaarifa.

Image caption Nokia E7 ni mojawapo ya simu tatu mpya zilizozinduliwa na kampuni hiyo ya Finland kwa matumaini ya kurejesha heshma.

Baadaye mwaka huu, Nokia inatarajiwa kutangaza simu nyingine zinazotumia mfumo wa MeeGo, ambazo wachambuzi wanadhani zitakuwa na mvuto zaidi kushindana na iPhone na simu zinazotumia mfumo wa Android.