Nokia na Apple zimeafikiana

Miaka miwili iliyopita Nokia iliifikisha kampuni ya Apple mahakamani nchini Marekani, ikidai kuwa imeiba ubunifu wake katika teknolojia ya kubofya juu ya scrini, kitambusho cha wito na Wi Fi.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Nokia ilitumia ubunifu wa Apple

Baadaye kampuni ya Apple nayo ikaijibu Nokia kwa kuishtaki. Makubaliano ya sasa yanamaliza mvutano wote wa kisheria uliokuwepo.

Inaonekana kuwa ni ushindi kwa Nokia kwani Apple imekubali kulipa mabilioni ya fedha na pia kuendelea na malipo yake ya tozo. Kiasi kamili cha fedha hakijatolewa.

Lakini makubaliano ya kisheria yanaonekana hayatabadilisha chochote katika soko ambako simu za kisasa za Nokia zinakabiliwa na ushindani mkubwa kuzidi simu za Apple na zingine za mkononi zinazofanya kazi kwa kutumia vifaa vya Google.

Katika taarifa yake yenye uangalifu mkubwa wa maneno, Apple imekubali kufikia makubaliano ya kileseni na Nokia lakini ikidai kuwa hayakidhi ukubwa wa ubunifu wake, ikisema kuwa, unaoifanya iPhone kuwa ya kipekee.

Haki miliki ya picha PA
Image caption tofauti na simu nyingine

Kwa maneno mengine ina maana kuwa Apple inakataa kuiba teknolojia ya inayoifanya iPhone ifanye vyema sokoni.