Huwezi kusikiliza tena

Emmanuel Jal mjini London

Image caption Jal alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC kuhusiana na juhudi zake za kuwasaidia watoto Afrika

Akiwa mjini London katika shughuli na mipango ya kukusanya fedha kwa niaba ya watoto katika shule mbalimbali barani Afrika, mwanamuziki wa Sudan Kusini, Emmanuel Jal, ambaye makazi yake ni Marekani, aliitembelea Idhaa ya Kiswahili ya BBC na kuzungumza na Ng'endo Angela.

Jal, akizungumza katika matangazo ya Dira ya Dunia ya Alhamisi, tarehe 05 Aprili, mbali na kuzungumza kuhusu juhudi za kuwasaidia watoto, alizungumza pia juu ya hali ya maisha katika Sudan ya Kusini, na mabadiliko yaliyojitokeza tangu nchi kujitenga kutoka Sudan na kuwa taifa huru.