Huwezi kusikiliza tena

Wamama wa DRC wajikwamua kiuchumi

Nchini DRC mtandao wa kutoa mikopo maeneo ya vijinini ambao umekuwa ukiwasaidia akina mama kuanzisha biashara sasa umetimiza mwaka mmoja huku riba inayotoka na mzunguko wa mikopo zikianza kulipwa kwa wanachama.

Wakati wanapoendelea kupata mafunzo na msaada wa kitaalam kutoka shirika moja la Kimataifa, wanawake hao wamekuwa wakitumia fedha zao.

Mradi huu uko Kivu ya Kusini.