Huwezi kusikiliza tena

Mji wa kale wa Timbuktu uko hatarini

Kundi la Ansar Dine linalodaiwa kushirikiana na mtandao wa Al Qaeda lidhibiti mji wa Timbuktu mapema mwaka huu. Kisha likaanza kuharibu makaburi ya kale kwa kisingizio kwamba yamejengwa kinyume na sharia.

Msemaji wa Ansar Dine Sanda Ould Bamana amethibitisha kwamba kundi lake limeharibu asili mia 90 ya makaburi yote ya kale ambayo hayajajengwa kwa misingi ya sharia la kiisilamu.

Amesema sharia haikubali makaburi yaliyojengwa zaidi ya urefu wa inchi sita.Shirika la kimataifa la Sayansi na Utamaduni limeomba serikali ya Mali kuzima kampeini za Ansar Dine.

Sidi Yahia ni moja wapo ya misikiti mikubwa zaidi ya Timbuktu.

Mlango wake ambao umevunjwa ilifungwa daima kwani ulikua kiingilio cha makaburi matakatifu ya mashahidi.Baadhi ya walioshuhudia uharibifu huo walianza kububujikwa na machozi.

Wakaazi wanaamini kuharibu makaburi hayo yataleta mkosi mkubwa.

Timbuktu ina sifa zake kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha imani ya kiisilamu katika karne zilizopita. Sifa zake kimataifa ni hususan misikiti mitatu mikubwa iliyojengwa karne za 15 na 16.Timbuktu pia wametoka mashahidi 333 wa dhehebu la Sufi la kiisilamu.

Ansar Dine ambao wanafuata dhehebu la Salafist limelaani heshima ya mashahidi. Kundi hilo liliteka Timbuktu Aprili baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Mali.

Awali kundi hili lilishirikiana na waasi wa Tuareg kutaka uhuru wa Kaskazini mwa Mali, lakini katika siku za karibuni makundi hayo yalitofautiana na sasa kundi la kiisilamu linadhibiti maeneo matatu muhimu ya Mali ikiwemo Timbuktu, Gao na Kidal.