Huwezi kusikiliza tena

Wakimbizi wa Burundi Tanzania taabani

Serikali ya Tanzania imetangaza kuwavua hadhi ya Ukimbizi raia zaidi elfu thelathini na saba wa Burundi ambao wamekuwa wakiishi nchini humo kama wakimbizi kwa zaidi ya miaka 19.

Serikali inasisitiza kuwa imefikia uamuzi huo baada ya kuridhika kuwa sababu zilizowafanya kuikimbia nchi yao ya asili,hazipo tena kwa sasa,na kwa maana hiyo hawana sababu za kuendelea kukaa uhamishoni nchini Tanzania.

Wakimbizi hao ambao bado wako kambini wanaendelea kuwa na wasiwasi hasa baada ya serikali kupeleka wanajeshi katika kambi hiyo wakati wakimbizi hao wakitarajiwa kufukuzwa kutoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu.

Serikali za Tanzania na Burundi pamoja na shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, wanasisitiza kuwa ni salama kwa wakimbizi hao kurejea makwao ambako walikimbia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya tisini.

Kambi hiyo inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 36,000 , itafungwa kabisa ifikapo mwezi Disemba.