Vurugu za mombasa baada ya kifo cha Aboud Rogo

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 16:44 GMT

Mombasa vurugu

  • Ghasia zilizozuka baada ya kuuawa kwa mhubiri mashuhuri mjini Mombasa Aboud Rogo. Vurugu zilitokea siku mbili mfululizo katika maeneo ya Mombasa mjini.
  • Polisi wa kupambana na ghasia walilazimika kushika doria ghasia zilipozuka ingawa sasa wanasema hali imedhibitiwa.
  • Makanisa yalivamiwa na kuporwa katika mji huo ambao una idadi kubwa ya waisilamu
  • Rogo alikuwa anasafiri kwenye gari hili na familia yake wakati aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana kwa mujibu wa polisi.Wafuasi wake wanadai kuwa alikuwa mwathirika wa mauaji ya kupangwa na hivyo wamewalaumu maafisa wa usalama.
  • Maiti ya Aboud Rogo ikibebwa na raia katika barabara kuu ya Mombasa kuelekea Malindi siku ya Jumatatu.
  • Baba mkwe wa Rogo' alinusurika mauaji hayo yaliyofanywa saa za mchana akiwa na mwanawe ambaye ni mke wa marehemu Rogo pamoja watoto wao
  • Mnamo mwaka 2005, mahakama moja ilimwondolea mashtaka marehemu Rogo ambaye umoja wa mataifa pamoja na Marekani wanamtuhumu kwa kufadhili kundi la wanamgambo la Al Shabaab na vile vile kushambulia hoteli ya Israel mjini Mombasa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.