Huwezi kusikiliza tena

Mgomo wa walimu nchini Kenya

Walimu nchini Kenya hii leo hawatafika madarasani wakati shule zikifunguliwa kwa muhula wa tatu wote wakigoma kuitaka serikali kutimiza ahadi yake ya miaka kumi na tano ya kuwaongeza mishahara na kuwapa mazingira bora ya kazi.

Mgomo huo utahusisha waalimu wa shule za misingi na sekondari licha ya Mahakama ya Viwanda nchini kuuharamisha.

vyama vya walimu wa shule za msingi (KNUT) na wale wa shule za sekondari (KUPPET) vinasisitiza kuwa mgomo huo bado upo kuanzia siku ya leo.

Na ili kufahamu zaidi kuhusu mgomo huo Ann Mawathe amezungumza na mwenyekiti wa chama cha walimu nchini Kenya bwana Wilson Sossion