Mgomo wa walimu nchini Kenya

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 09:48 GMT

Media Player

Mgomo huo utahusisha waalimu wa shule za misingi na sekondari licha ya Mahakama ya Viwanda nchini kuuharamisha

Sikilizamp3

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Walimu nchini Kenya hii leo hawatafika madarasani wakati shule zikifunguliwa kwa muhula wa tatu wote wakigoma kuitaka serikali kutimiza ahadi yake ya miaka kumi na tano ya kuwaongeza mishahara na kuwapa mazingira bora ya kazi.

Mgomo huo utahusisha waalimu wa shule za misingi na sekondari licha ya Mahakama ya Viwanda nchini kuuharamisha.

vyama vya walimu wa shule za msingi (KNUT) na wale wa shule za sekondari (KUPPET) vinasisitiza kuwa mgomo huo bado upo kuanzia siku ya leo.

Na ili kufahamu zaidi kuhusu mgomo huo Ann Mawathe amezungumza na mwenyekiti wa chama cha walimu nchini Kenya bwana Wilson Sossion

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.