Huwezi kusikiliza tena

Ulemavu sio kikwazo kwa Jaji wa Kenya

Mashindano ya Olimpiki ya walemavu yanayoendelea mjini London Uingereza ni dhihirisho tosha kuwa ulemavu sio kikwazo cha mafanikio kwa mwanadamu.

Kutana na Jaji wa mahakama ya rufaa nchini Kenya Daniel Aganyanya. Aliugua ugonjwa wa kupooza wakati akiwa na umri wa mwaka mmoja na kisha kuwa mlemavu.

Jaji Aganyanya alistaafu mwezi Januari baada ya kuhudumu katika idara ya mahakama kwa zaidi ya miaka thelathini licha ya ulemavu wake. Anatuelezea kuhusu maisha yake kama jaji.