Huwezi kusikiliza tena

Rwanda tayari kutuma vikosi DRC

Mkutano wa viongozi wa mataifa ya maziwa makuu kuhusu usalama wa Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaanza leo nchini Uganda.

Ingawaje mojawapo wa njia zinazodhaniwa kutoa suluhisho kwa mgogoro wa Mashariki mwa Congo ni kuunda kikosi cha kulinda amani huko, kuna taarifa kuwa Congo haitaki baadhi ya nchi kuchangia.

Rwanda imesema iko tayari kutuma majeshi yake katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani kinachopendekezwa ili kumaliza mzozo wa mashariki mwa Congo.

Rwanda imetoa kauli hiyo licha ya taarifa kuwa Jamuhuri ya Kidemkrasia ya Congo ingependelea baadhi ya nchi kutohusika katika mpango huo.

Msemaji wa jeshi La Rwanda Brigedia generali Nzabamwita amesema hayo kabla ya mkutano wa viongozi wa maziwa makuu kuhusu usalama wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,utakaofanyika mjini Kampala Uganda. Alizungumza na Siraj Kalyango