Huwezi kusikiliza tena

Wasomali wa Kibantu. Maisha yao ng'ambo

Wasomali wenye asili ya Kibantu, ambao mababu zao wametokea Tanzania na Msumbiji wana tofauti ya kimaumbile, na hata kitamaduni na Wasomali wa kawaida.

Baada ya kukimbia mapigano nchini Somalia katika miaka ya 90, walijikuta katika kambi za wakimbizi nchini Kenya. Mwaka 2003, Marekani ilikubali kuchukuwa wakimbizi elfu 13, katika kile kilichoelezwa na mamlaka za Marekani kuwa mpango mkubwa wa uhamishaji watu kutoka Afrika.

Lakini hata hivyo haijakuwa safari rahisi, kama ambavyo Salim Kikeke aliposhuhudia alipokwenda huko hivi karibuni.