Huwezi kusikiliza tena

Rwanda na vita vya DRC

Makundi ya kiraia na yale ya kidini katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yanalaumu jamii ya kimataifa yakisema imeshindwa kuchukua hatua yoyote kuhusiana na madai ya Rwanda kuhusika katika kuwasaidia waasi wanaopigana na vikosi vya serikali mashariki mwa nchi hiyo.

Mapema mwaka huu umoja wa mataifa ulitoa ripoti ya uchunguzi iliyodhihirisha kwamba Rwanda imekuwa ikiwapa silaha makundi ya waasi, lakini Rwanda imekanusha madai hayo.

Makundi ya kiraia na kidini yamekusanya sahihi kutoka zaidi ya watu milioni moja na kuwasilisha hoja mbele ya umoja wa mataifa, kutaka hatua kuchukuliwa.

Hoja hiyo ilipelekwa New York na Askofu wa jimbo la Kindu mashariki mwa Congo Katanda Masimango, na akapitia London. Zuhura Yunus alizungumza naye kuhusu hoja yao.