Rwanda na vita vya DRC

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 17:38 GMT

Media Player

Makundi ya kiraia DRC yalaumu jamii ya kimataifa kwa kutochukua hatua kuhusu madai ya Rwanda kujihusisha na vita DRC

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Makundi ya kiraia na yale ya kidini katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yanalaumu jamii ya kimataifa yakisema imeshindwa kuchukua hatua yoyote kuhusiana na madai ya Rwanda kuhusika katika kuwasaidia waasi wanaopigana na vikosi vya serikali mashariki mwa nchi hiyo.

Mapema mwaka huu umoja wa mataifa ulitoa ripoti ya uchunguzi iliyodhihirisha kwamba Rwanda imekuwa ikiwapa silaha makundi ya waasi, lakini Rwanda imekanusha madai hayo.

Makundi ya kiraia na kidini yamekusanya sahihi kutoka zaidi ya watu milioni moja na kuwasilisha hoja mbele ya umoja wa mataifa, kutaka hatua kuchukuliwa.

Hoja hiyo ilipelekwa New York na Askofu wa jimbo la Kindu mashariki mwa Congo Katanda Masimango, na akapitia London. Zuhura Yunus alizungumza naye kuhusu hoja yao.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.