Huwezi kusikiliza tena

Sudan mbili zimeafikia nini?

Sudan na Sudan Kusini: Nchi hizi mbili zimekuwa zikizozania mpaka na mapato ya mafuta tangu mwezi Januari mwaka huu.

Wakati wa mgogoro huu,Sudan Kusini ilifunga mabomba yake ya kusafirishia mafuta na kisha kusitisha uzalishaji wa mafuta hayo. Kitendo ambacho, kilikuwa na athari kubwa kwa uchumi wake.

Serikali imetumia pesa zake za zote kigeni na kuiacha nchi hiyo ikitegemea sana mikopo. Serikali kwa sasa inaomba moko wa dola milioni miambili kutoka kwa benki moja ya kimataifa miezi minne tu baada ya kuomba mkopo wa kiasi hicho kutoka kwa benki ya taifa ya Qatar.

Nyambura Wambugu anasimulia mustakabali wa nchi hzi mbili ikiwa zitaweza kuafikiana.