Huwezi kusikiliza tena

Ndani ya mapango Zanzibar

Kwa muda mrefu imekuwa ikiaminika kuwa makazi ya watu wa pwani ya Afrika Mashariki yalianza baada ya kuwasili kwa wageni waliofika kufanya biashara na wenyeji kutoka Mashariki ya Kati na mbali.

Lakini kuna ushahidi wa kutosha kubadilisha mtizamo huo.

Baada ya kufukua pango moja nje ya mji wa Zanzibar, wataalam wamegundua ushahidi wa makazi kuwepo hapo na wanyama wa kufugwa na shughuli za kibiashara miaka 3000 kabla ya kristo.

Hassan Mhelela amefika katika pango la Kuumbi na kutuandalia taarifa hii.