Huwezi kusikiliza tena

Maskini wapokea 'Smart Card' Kenya

Katibu mpya wa shirika la misaada la Uingereza, Justine Greening, ameahidi kuhakikisha kuwa misaada ya shirika hilo inatolewa kwa lengo la kuizia majanga ya baadaye katika Upembe mwa Afrika.

Watoto wa Afrika ambao wanakabiliwa na njaa, watapokea takriban pauni milioni kumi na saba kutoka kwa pesa za umma nchini Uingereza ikiwa ni sehemu ya msaada wa nchi hiyo zinazotumiwa katika mpango maalum wa kupunguza njaa.

Tangazo hilo lilitolewa wakati Bi Greening alitembelea moja ya miradi ambayo shirika hilo linafadhili, kukabiliana na njaa Kaskazini mwa Kenya

Jamii ambazo ni maskini sana katika eneo hilo, zinapokea pesa moja kwa moja kutoka kwa wafadhili bila kupitishia mikononi mwa serikali.