Ukombozi wa Kismayo

Imebadilishwa: 4 Oktoba, 2012 - Saa 15:56 GMT

Picha za Kismayo

 • Wanajeshi wa AMISOM wakiwa tayari kuukomboa mji wa Kismayo kutoka mikononi mwa Al Shabaab
 • Wanajeshi wa AMISOM waliuzingira mji wa Kismayo kutoka pande zote tayari kwa mashambulizi ya ardhini na angani.
 • Majeshi ya AMISOM yamekuwa yakiuzingira mji wa Kismayo kutoka pembe zote na hata kutoka angani. Haya ni maeneo yanayopakana na mji huo kutoka upande wa Kenya
 • Walitumia vifaru na helikopta za kijeshi kufanya utafiti wao kabla ya kuingia katikati mwa mji huo.
 • Mji wa bandarini wa Kismayo tayari kukombolewa
 • Jeshi la Kenya kwa ushirikiano na majeshi ya AMISOM, limekuwa likikabiliana na Al Shabaab ambao ngome yao ya mwisho ilikuwa Kismayo hadi walipofurushwa kutoka mjini humo mapema wiki hii.
 • Baadhi ya sehemu ambazo majeshi hayo yalidhibiti kwanza ni chuo hiki kikuu cha Kismayo, uwanja wa ndege na sehemu zengine za umma kabla ya kuingia katikati mwa Kismayo.
 • Chuo kikuu cha Kismayo kilichokombolewa.
 • Walitumia mbinu zote kupambana na Al Shabaab ikiwemo helikopta za jeshi
 • Kabla ya kuufikia mji wa Kismayo wanajeshi hawa walikuwa na kibarua cha kufanya mkakati ambao haungeleta madhara kwa wenyeji wa Kismayo kutokana na makabiliano yoyote. Hapa wanapumzika
 • Tayari kwa mapambano, vikosi vya AMISOM vikiwa kwenye kifaru hiki kuelekea Kismayo

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.