Huwezi kusikiliza tena

Ni uamuzi wa kihistoria

Mahakama Kuu nchini Uingereza imeamua kuwa wakenya watatu walioteswa chini ya serikali ya Ukoloni miaka ya hamsini, wanaweza kuishtaki Uingereza ili walipwe fidia.

Jaji Richard McCombe, alisema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha mateso yalitokea kwani serikali ya Uingereza wakati huo ilikuwa makini sana katika kuweka rekodi za yaliyotokea.

Akizungumza punde tuu baada ya uamuzi huo wa Mahakama kutolewa, mojawapo ya mawakili ya wakenya hao, Gitobu Imanyara ameelezea furaha yake na kutaja kesi hiyo kama ya kihistoria.