Afrika wiki hii kwa picha

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2012 - Saa 14:01 GMT

Picha Afrika

 • Mamia walijitokeza kumkaribisha Rais Omar al-Bashir katika uwanja wa ndege mjini Khartoum Ijumaa alipokuwa anarejea kutoka Ethiopia baada ya kutia saini makubaliano na Sudan Kusini kuhusu, mafuta, biashara na usalama na hivyo kupunguza hali ya taharuki kati ya nchi hizo mbili.
 • Katika siku hiyo pia, hali ya wasiwasi ilikumba mji mkuu wa Guinea ,Conakry, hali ilikuwa hivyo, wakati wa mazishi ya wafuasi wawili wa upinzani waliouawa katika ghasia za hivi karibuni zilizowahusisha polisi.
 • Watu katika mji wa Benghazi nchini Libya, waliunda utepe kwa kutumia foleni ya watu hapa ambao ni ishara ya kupambana na saratani ya matiti wakati wa siku ya kuhamasisha kuhusu saratani ya matiti duniani.
 • Wanamitindo wakionyesha umbo zao mjini Lagos siku ya Jumamosi, mshindi wa shindano hilo atashiriki katika shindano lengine la fainali la Elite Model, baadaye mwezi huu nchini China
 • Mjini Lagos siku nne baadaye, mfanyakazi wa kampuni ya umeme alionekana hapa akitengeza nyaya za stima. Wenyeji wa mji mkubwa zaidi Kusini mwa jangwa la Sahara, mara kwa mara hulalamika kuhusu mpango duni wa kusambaza umeme Mjini Lagos
 • Watu walioathirika kutokana na mafuriko yanayoendelea katika jimbo la Kogi, hapa wanasafiri kwa boti, kutafuta hifadhi katika mji wa Idah
 • Mnamo siku ya Jumatano, mwalimu katika mji wa Idah anafunza wanafunzi katika darasa la muda katika kambi ya watu waliotoroka mafuriko. Duru zinasema kuwa takriban watu 10,000 wameachwa bila makao kutokana na mafuriko yanayosemekana kuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa.
 • Siku ya Jumanne, wapiganaji wa Ras Kamboni,wanaounga mkono majeshi ya Somalia, wanashirikiana na majeshi ya Muungano wa Afrika kuelekea katika mji wa Kismayo katika harakati zao dhidi ya Al-Shabaab
 • Siku iliyofuata, washukiwa wa Al-Shabab walikamatwa mjini Kismayo na kupewa ulinzi mkali na majeshi ya serikali karibu na kituo kimoja cha polisi.
 • Hapa polisi huyu yuko mbele ya lori lililowashwa moto na madereva wa malori waliogoma karibu na barabara kuu kuelekea Cape Town, Afrika Kusini. Takriban madereva 20,000 wanataka nyongeza ya mishahara, inaarifiwa kuwa mgomo huo tayari umeanza kuathiri usambazaji wa mafuta nchini humo
 • Siku iliyofuata wafanyakazi wanasafisha chemichemi ya maji katika msikiti mjini Johannesburg baada ya kufunguliwa rasmi na rais Jacob Zuma. Ni msikiti mkubwa zaidi katika kanda ya Afrika Kusini.
 • Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete,anabebwa katika gari la farasi katika mji mkuu wa Canada, Ottawa chini ya ulinzi wa polisi Ottawa, wakati wa ziara rasmi.
 • Katika ziara nyingine ya kimataifa, Rais wa Gabon Ali Ben Bongo hapa na mwenzake wa Cuba, Raul Castro katika ikulu ya Rais mjini Havana siku ya Ijumaa wakati alipokuwa anakaribishwa rasmi katika kisiwa hicho cha Caribbean.
 • Mnamo siku ya Alhamisi, watoto waliwaachilia huru njiwa katika mji mkuu wa Msumbiji Maputo, kuadhimisha miaka 20 tangu mkataba wa amani kufikiwa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 16. Nchi hiyo ni mojawapo ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa kiuchumi barani Afrika.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.