Huwezi kusikiliza tena

Mustakabali mwema kwa Somalia

Mapema wiki hii majeshi ya AMISON yaliuteka mji wa Kismayo ambayo ilikuwa ngome kuu ya Al-Shabaab na hivyo kutoa matumaini makubwa kuwa Somalia huenda ikawa nchi thabiti.

Kufuatia hatua hiyo mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustin Mahiga, alisema kwamba Umoja wa Mataifa inajiandaa kuhusika zaidi na maswala ya Somalia ili kusaidia nchi hiyo katika mustakabali wake.

Alitoa kauli hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi, Kenya.