Huwezi kusikiliza tena

Kesi ya Mau Mau kuendelea

Mahakama kuu imetoa uamuzi kwamba Wakenya watatu wakongwe walioteswa chini ya utawala wa ukoloni wa Waingereza zaidi ya miaka 60 iliyopita wanaweza kuendelea na kesi yao ya kutaka kulipwa fidia na serikali ya Uingereza.

Serikali ya Uingereza ilikuwa imekiri wapigania uhuru hao, wakati huo wakiwa wanachama wa vuguvugu la Mau Mau walifanyiwa ukatili.

Uingereza imejitetea kwa kusema, miaka mingi imepita tangu kutokea matukio hayo, na kwa hivyo haiwezekani kuwa na kesi ya haki. Hata hivyo Jaji ameamua kuwa kuna ushahidi wa kutosha kwenye nyaraka zilizohifadhiwa tangu zama hizo. Peter Musembi alikuwepo mahakamani.