Huwezi kusikiliza tena

Ongezeko la watu Uganda

Uganda ina ongezeko kubwa la watu duniani. Kiwango cha uzazi cha nchi hiyo kwa sasa ni watoto 5.9 kwa kila mwanamke. Idadi ya watu wa Uganda imeongezeka tangu mwaka 1960 ambapo watu walikuwa milioni 6.6. Kwa sasa nchi hiyo ina jumla ya watu milioni 34.5. Ifikapo mwaka 2050 Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa idadi hiyo itakaribia watu milioni 100 ambayo ni mara tatu ya idadi ya sasa.

Mwandishi wetu Idd Seif anaripoti kutoka Kampala.