Huwezi kusikiliza tena

Njama ya wabunge yatibuka Kenya

Rais wa Kenya Mwai Kibaki, amekataa kuidhinisha mipango ya wabunge wa taifa hilo kujipatia kitita kikubwa cha pesa kama marupurupu ya kuhudumu kama wabunge.

Wabunge hao walipanga kujilipa dola alfu mia moja na kumi kila mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Lakini bwana Kibaki amesema kuwa hatua hiyo inakiuka katiba na haiwezi kutekelezwa wakati ambapo walimu pamoja na madaktari nchini Kenya wamekuwa wakigoma kudai nyongeza ya mishahara. Wananchi walijitokeza katika barabara za mji wa Nairobi kulaani hatua ya wabunge hao.