UN imekosa wa kumlaumu

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 17:05 GMT

Media Player

Rwanda na Uganda zimekana madai yanayotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu kuunga mkono M23

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Kwa mara nyingine tena Rwanda na Uganda zimekana madai yanayotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu kuwaunga mkono waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Uganda inasema umoja huo unatafuta mtu wa kumlaumu kwa kushindwa kwa jeshi lake mashariki mwa Congo.

Ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa iliyoonekana na shirika la habari la Reuters imesema majeshi ya Rwanda na Uganda yamewapatia silaha waasi

Salim Kikeke amezungumza na balozi wa Rwanda hapa Uingereza Ernest Rwamucyo na kutaka kufahamu wanajibu vipi tuhuma hizi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.