Kimbunga Sandy chakaribia kupiga

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 15:32 GMT

Kimbunga Sandy

  • Kimbunga Sandy kilianza kupiga kutoka nchini Cuba wiki iliyopita ambako ilisababisha vifo vya watu karibia ishirini
  • Mji wa New York umesemekana kuwa katika hatari ya kuathirika pakubwa kufuatia kimbunga hiki kwa kuwa mji huo unazungukwa na maji
  • Mashirika ya ndege yalilazimika kusitisha safari kwa hofu ya dhoruba kali kwa hivyo waliofika kwenye viwanja vya ndege walilazimika kurejea nyumbani. Hapa watu wanakimbilia usalama wao mjini New York
  • Magunia ya mchanga yaliwekwa kando ya maji ili kuhimili mawimbi makali lakini watu hawakujizuia na shughuli za kuvinjari maeneo hayo
  • Sehemu nyingi za mji zilifurika maji lakini watu waliendelea na shughuli zao ingawa kwa tahadhari
  • Soko la hisa la New York lilifunga kazi
  • Sehemu na makaazi ya watu na mikahawa karibu na maeneo ya maji zilionekana kuathirika mwanzo kwa mawimbi makali kisha maji
  • Hii ndiyo picha iliyotolewa na idara ya utabiri wa hali ya hewa kutahadharisha watu kuhusu mawimbi na dhoruba iliyokuwa inakuja.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.