Ulemavu wangu sio hoja

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 13:55 GMT

Mlemavu wa Naivasha

  • Ni katika mtaa mmoja mjini Naivasha ambako Godfrey Ipalei mwenye umri wa miaka 44 anaishi peke yake. Hana mke lakini hashindwi kujifanyia kazi zake mwenyewe kwani hajioni kama mlemavu.
  • Hujifanyia usafi nyumbani bila msaada wa mtu yeyote na anasema hawezi kujifananisha na walemavu kwani mtu mlemavu hawezi kujifanyia chochote.
  • Hapa anajiandaa kutayarisha maji ya moto na kwa hivyo itambidi achukue kiberiti na kuwasha jiko lake la gesi. Na hivi ndivyo yeye hufanya kila asubuhi anapotaka kwenda kazini na jioni anaporejea nyumbani katika kujiandalia chakula chake
  • Yeye hutumia sehemu za mikono yake ambazo hazina vidole kuwasha jiko wakati akichemsha maji yake au hata kujipikia.
  • Na je hufanya je wakati akitoa maji kwenye jiko lake?
  • Wengi ambao hawana ulemavu humuona Ipalei kama mtu asiyejiweza lakini hakosi kujilisha wala kijinywisha kwa hali mikono yake ilivyo
  • Utajiuliza labda Ipalei hutumia vipi simu yake ya rununu? Sio hoja kwake kwani ni rahisi kama abc...
  • Ipalei ni mtaalamu wa komputa na ana komputa yake maalum ambayo huitumia kwa kazi zake binafsi
  • Hiki ni chuo anuai cha mafunzo ya komputa ambacho Ipalei hufunza. Hutumia taaluma yake , kuwaelimisha wanafunzi kuhusu matumizi mbali mbali ya komputa.
  • Ipalei ameandika kitabu kuhusu ulemavu na changamoto zake lakini kichwa cha kitabu chake kinasema yeye sio mlemavu na hajioni kama mlemavu kwani hakuna asichoweza kufanya. Bila shaka anawapa watu wengi walio na ulemavu matumaini ya kuishi maisha ya kawaida

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.