Kampeini zapamba moto Marekani

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 08:38 GMT

Kampeini za uchaguzi Marekani zapamba moto

 • Raia wa Marekani walimuunga mkono kwa wingi Rais Obama miaka minne iliyopita lakini baada ya hapo sio msukosuko tu wa uchumi bali pia ushawishi wake kwa wamarekani waliomuunga mkono miaka minne iliyopita imeshuhudiwa nchini humo
 • Mgombea wa Republican na mshindani mkubwa wa Barack Obama amekuwa akinufaika kutokana na ushawishi aliopoteza Rais Obama huku kura za maoni zikionyesha wawili hao kukaribiana kwa ushawishi
 • Mitt Romney na mkewe wakiwasili katika mojawapo ya majimbo wanakoeendesha kampeini zao za mwisho mwisho kabla ya uchaguzi siku ya Jumanne
 • Michelle Obama mkewe Rais Barack Obama alihudhuria kampeini na za mumewe na kuwataka wanawake kumuunga mkono
 • Baadhi ya wamarekani walioamua kutomuunga mkono Rais Obama wakisema hawajaridhishwa na uongozi wake
 • Bill Clinton ambaye pia ni rais wa zamani wa Marekani amekuwa katika msitari wa mbele kumpigia debe Rais Obama, katika kempeini zake na Obama amemsifia sana kwa namna anavyoelezea maswala tata kwa wananchi kuhusu utawala wa weke ambayo labda watu hawaelewi
 • Bango hili ni ishara ya mojwapo ya mambo ambayo yalileta utata katika siasa za Marekani. Balozi wa nchi hiyo nchini Libya aliuawa kufuatia mashambulizi ya kigaidi na watu walikosoa sana utawala wa Obama kwa kukosa kuweka ulinzi wa kutosha katika balozi za Marekani duniani.
 • Romney hapa akionekana na watoto ambao ni sehemu ya wale wanaomuunga mkono kwao lenye umuhimu ni sera ya masomo na baada ya masomo watapata vipi ajira.
 • Mfuasi huyu wa Obama hapa anaonekana kujitolea katika kuonyesha kuwa yuko katika msitari wa mbele kuhakikisha Obama anapata muhula mwingine uongozini.
 • Mit Romney akionekanja hapa kumkumbatia mtoto mdogo wakati kampeini zake zikiendelea
 • Huyu ni mfuasi sugu wa Rais Barack Obama

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.