Wamarekani wafika kwenye debe

Imebadilishwa: 6 Novemba, 2012 - Saa 10:16 GMT

Uchaguzi umeanza Marekani

  • Hatimaye wamarekani wataweza kujua mbichi na mbivu katika uchaguzi mkuu wagombea Obama na Mit Romney wakitoana jasho. Foleni hii ya wapiga kura waliofika hapa mapema kuweza kumchagua kiongozi wampendaye.
  • Moja ya vyumba vya kupigia kura
  • Mpiga kura huyu alikuwa miongoni mwa wale waliojitokeza kupiga kura asubuhi na mapema
  • Mashine hizi ni za kisasa za kupigia kura kwenye uchaguzi huu
  • Wagombea walijitokeza kimasomaso kuwaomba kura wananchi na hata kyungana nao katika kampeini za mwishomwisho kabla ya kuanza kwa uchaguzi
  • Moja ya mabango ya kampeini za uchaguzi huo hii ikimlenga Mit Romney ambaye anasifika kama tajiri mkubwa asiyejua hali ya mmarekani wa kawaida na wa kipato cha chini
  • Hawa ni baadhi ya watu waliokerwa na shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Libya na kusababisha kifo cha balozi Stevens. Baadhi ya wamarekani walilaumu sana utawala wa Obama kwa kupuuza usalama wa maafisa wake ughaibuni
  • Bendera hizi ni ishara ya uzalendo wa wamarekani wakati wa uchaguzi huu
  • Mfanyabiashara huyu alichukua nafasi hii kujitafutia mapato kwa kuuza t-shirts za kumpigia debe rais Obama
  • Haya ni makao makuu ya kampeini za Barack Obama

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.