Afrika Wiki hii

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 17:43 GMT

Afrika Wiki hii

 • Mashabiki wakishangilia kwenye tamasha ambalo wanamuziki Alpha Blondy na Tiken Jah Fakoly walishiriki katika mji mkuu Abidjan siku ya Jumamosi. Maafisa wa utawala wanaanda wanamuziki hao ambao ni mahasimu kuzuru nchi hiyo wakifanya tamasha kama njia ya kuwapatanisha baada ya miaka mingi ya uhasama wa kisiasa pamoja na mizozo.
 • Wanawake waliovalia nguo za chama tawala nchini Cameroon wakionekana kuonyeshana kitu wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 30 za utawala wa Rais Paul Biya
 • Mjini Rutshuru, Mashariki mwa DRC, eneo lililo chini ya udhibiti wa waasi walioondoka jeshini , mwanamke akinunua samaki siku ya Jumamosi
 • Siku hiyohiyo mwanamume anaonekana kuuza Petroli mjini Rutshuru kwenye chupa kando ya barabara
 • Siku ya Jumatatu mganda wa kienyeji John Dimo ambaye ni mwanajeshi wa zamani, anayeshukiwa kuwa na miaka 100, anapiga ramli kutabiri kuwa Barack Obama angeshinda uchaguzi mkuu uliokamilka Jumatano . Bwana Dimo ambaye bila shaka hakukosea anaishi katika kijiji cha Kogelo alikozaliwa babake Obama
 • Siku mbili baada ya kuchaguliwa kwa Obama, mwenye duka la magazeti haya mjini Casablanca nchini Morocco, anapanga magazeti yake yenye habari za ushindi wa Obama
 • Mcheza soka wa Gabon, Pierre-Eme Aubameyang anasherehekea kuingizia bao kilabu yake ya Ufaransa, Saint-Etienne siku ya Jumamosi wakati wa mechi dhidi ya kilabu ya Paris Saint-Germain.
 • Mwanaume anamrekodi Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf akitoa hotuba ya kupokea tuzo lake alilopewa la (Grand Cross of Legion of Honour) kando ya Rais wa Ufaransa Francois Hollande wakati wa sherehe zilizofanyika siku ya Jumatano.
 • Mnamo Ijumaa, shabiki wa Tennis nchini Nigeria anamshikia bango mcheza tennis Serena Williams mjini Lagos. Madada wawili Serena na Venus walikuwa katika ziara ya nchi mbili barani Afrika, Nigeria na Afrika Kusini.
 • Wanajeshi wa Afrika Kusini kwenye gwaride mjini Cape Town kumkaribisha Rais wa nchi jirani Namibia Hifikepunye Pohamba
 • Siku hiyo hiyo, waisilamu wa madhehebu ya Salafi nchini Tunisia waliandamana nje ya mahakama mjini Tunis, kutaka watu waliokamatwa baada ya kuhusishwa na shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani mwezi Septemba.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.