Mafuriko yasomba matumaini Nigeria

Imebadilishwa: 28 Novemba, 2012 - Saa 13:08 GMT

Mafuriko ya Nigeria

  • Mafuriko katika miezi ya hivi karibuni kote nchini Nigeria yamesababisha maafa ya watu 363 na kuwaacha mamilioni bila makao. Mfanyakazi huyu wa shambani Dalami katika jimbo la Rivers state,anasema kuwa siku ambapo mafuriko yalianza zaidi, mbuzi hamsini walizama.Mpiga picha Gideon Mendel alitembelea baadhi ya jamii zilizoathirika kutokana na mafuriko hayo.
  • “Mtoto wangu Godstimem alikuwa na mwaka mmoja na alisombwa na maji,” anasema Toinzbeze Nelson akimpakata mwanawe wa kike Destiny
  • Mwanamke huyu anatembea kwenye maji ya mafuriko, akielekea kanisani Jumapili asubuhi. Maeneo mengi ya jimbo la Bayelsa yamejaa maji, ikiwemo kijijini anakotoka Rais Goodlluck Jonathan
  • Wisdom na Lilian Ginikawa walikuwa na duka ndogo karibu na nyumba yao hapa Igbogeni. "tulilazimika kukimbia na kuacha kila kitu chetu,'' Ginikawa.
  • Florence Abraham,mwenye umri wa miaka 48, anasema alitoroka na watoto wake sita hadi katika maeneo salama.
  • ''Wakati maji yalipoanza kuingia kwenye nyumba yangu, niliona kama mzaha,'' anasema Godspower Kenz. ''Hatukujua kama maji yangefika kiwango hiki. Nimetupa vitu vyangu vingi vilivyoharibiwa katika mafuriko haya.'' Hatuna maji wala chakula'' alisema
  • Ratmas Ebiarohon, anaoga kwenye maji ya mafuriko katika eneo la Igbogeni. ''Mafuriko yalikuja kwa kasi.'' Nyumba yangu iliharibiwa vibaya. Mimi ni seremala, na vifaa vyangu nyote viliharibiwa pia.'' alisema Ratmas
  • Kingsley Isiakpere na mkewe Edna Silas, walio na watoto sita walisema walikuwa usingizini wakati maji yalipofika. ''Tulianza kukusanya vitu vyetu kwa haraka sana ,ikiwemo viti na meza zetu. Tumepoteza nguo na vifaa vyetu vya ujenzi.'' alisema bwana Isiakpere.
  • Mganga wa kienyeji Joseph Edem, mkewe Endurance na watoto wao Godfreedom,mwenye umri wa miaka 10 na Josephine mwenye umri wa miaka 12, wanasema kuwa mafuriko yalitokea ghafla . ''Nilidhani kifo kimefika ,'' alisema Josephine. ''Hata sijui waliko marafiki zangu.''
  • "Tulipoteza vitu vingi sana , hata siwezi kuhesabu. Mbu hutuuma kila siku na hatuna chakula cha kutosha hapa anasema bwana Nelson.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.