Wafungwa wafuzu kisheria Kenya

Imebadilishwa: 5 Disemba, 2012 - Saa 13:16 GMT

Wafungwa wa jela Kenya wapewa mafunzo ya kujiwakilisha mahakamani

 • Mwenyekiti wa kituo cha sheria akiwahutubia wafungwa waliofuzu.
 • Wafungwa wengine wakiwa kwenye sherehe huku askari jela akiwa anawalinda.
 • Magereza nchini Kenya yamekuwa na mwamko mpya na ushirikiano wa askari na wafungwa umeongezeka.
 • Mavazi kwenye jela za Kenya ni changamoto kubwa
 • Wafungwa wengine walipata nafasi ya kuwatumbuiza wenzao kwa miondoko ya kisasa
 • Nyimbo na kunengusha viungo ziliwapa wengine afueni kwa kuwaliwaza mawazo.
 • Wengine hawakuami wenzao wana tajiriba ya kudensi kiasi hicho.
 • Mmoja wa waliofuzu akionyesha jinsi ya kuapa katika mahakama wakati akijitetea.
 • Baadaye wafungwa waliofuzo walifanya mchezo wa kuigiza wa mahakama
 • Inakisiwa kuna wafungwa wengi walio jela kwa ajili ya ukosefu wa mawaidha ya kufana.
 • Susan Kangaha amekuwa jela kwa zaidi ya muda wa miaka sita kwa ajili ya ukosefu was jinsi ya kuwakilishwa katika kesi yake ya rufa.
 • Lebogang Sibanda ni mfungwa kutoka Afrika Kusini.Yuko jela kwa kupatikana na hatia ya kuwa na madawa na kulevya
 • Wafungwa wa gereza la kina mama la Langata,Nairobi wakiwa na vyeti vyao vya kufuzu baada masomo ambavyo watu wanawakilishwa mahakamani

Wafungwa wengi kote duniani hujipata wanasalia kuishi gerezani kwa kukosa uwakilishwaji mzuri wakati wa kesi zao.

Hata hivyo je anaweza kujiwakilisha mwenyewe hata kama atakuwa na elimu ya kisheria au lazima apata kusaidiwa?

Nchini Kenya shirika la kijamii ya kutoa misaada ya kisheria Kituo Cha Sheria, kimekuwa kikitoa mafunzo kwa wafungwa wanawake wa jela ya Langa'ata mjini Nairobi Kenya na kuwapa uelewa kuhusu sheria na wanavyoweza kujitetea mahakamani.

Picha zimepigwa na Peter Njoroge

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.