Tisho dhidi ya wanyamapori

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 10:03 GMT

Uhalifu dhidi ya wanyama pori

  • Kulingana na hazina ya kimataifa ya wanyamapori, biashara haramu inaendelea kutishia maisha ya wanyama kama Ndovu, Vifaru, na Chui wakubwa barani Afrika na hata Asia. Maelfu ya Ndovu huuwawa kila mwaka kwa sababu ya pembe zao na sasa ni chini ya Chui 3, 200 waliosalia mbugani
  • ''Ni jamii hasa hasa zile maskini duniani ambazo hupata hasara kubwa kufuatia uwindaji huu haramu wakati makundi ya wahalifu pamoja na maafisa wafisadi, hufaidika. Askari wa huduma za wanyamapori, wanapoteza maisha yao pamoja na riziki yao,'' anasema Jim Leape, mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la wanyamapori.
  • Licha ya marufuku ya miaka 23 ya biashara ya pembe za ndovu, ndovu wanaendelea kuuawa kwa sababu ya pembe zao.
  • Watetezi wa uhifadhi wa wanyamapori, wamerekodi idadi kubwa sana ya Ndovu wanaoendelea kuuawa barani Afrika.
  • Marufuku ya mwaka 1989, iliharamisha biashara ya pembe za ndovu , lakini mwaka 2008, China na Japan ziliruhusiwa kununua pembe haramu za ndovu zilizokuwa zimenaswa. Hii bila shaka inatatiza vita dhidi ya biashara haramu ya wanyama pori.
  • Watafiti katika idara ya usimamizi wa mbuga za kimataifa wanyamapori na mimea, wanafanyia utafiti pembe za ndovu zilizonaswa kubaini zilikotoka.
  • Pembe za ndovu hutumika kutengeza dawa za kienyeji pamoja na kutengeza mapambo ya vito
  • Adhabu ya hatia ya biashara haramu ya wanyama walio kwenye tisho la kuangamia ni kifungo cha miaka kumi jela, pamoja na kutozwa faini mara nne ya thamani ya vitu atakavyopatikana navyo mhalifu.
  • Afisaa mmoja anakagua duka la kuuza mapambo yaliyotengezwa kwa pembe za ndovu katika soko moja nchini Thailand.Julai mwaka 2012, takriban nusu tani ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola zaidi la yaki saba zilinaswa katika uwanja wa ndege wa Bangkok

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.