Picha za maandamano Misri

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 16:01 GMT

EGYPT

  • Wanajeshi wa Misri wanashika doria katika baadhi ya miji mikubwa ambapo maandamano yanafanyika kupinga au kuunga mkono kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba itakayofanyika siku ya Jumamosi
  • Wanajeshi wameruhusiwa kuchukua hatua dhidi ya waandamanaji watakaozua rabsha
  • Katika mji wa Alexandria ambao ni mji wa bandarini , wananchi asubuhi ya leo walianza kuandamana kuipinga katiba lakini polisi walikuwepo kuwazuia
  • Maandamano yalianza baada ya mhubiri mmoja katika msikiti mmoja kuwashauri waumini kupigia kura ya ndio katiba
  • Waandamanaji mahasimu hawajachoka tangu mapema wiki hii walipoanza kuandamana wakipinga katiba ya rais Morsi huku wengine wakiiunga mkono
  • Waandamanaji wengi wanasema kuwa wataipinga katiba hiyo
  • Hawakutaka kuondoka hata baada ya jeshi kuamrishwa kuwakamata wale watakaokiuka sheria, agizo ambalo wengi wamelitafsiri kama Misri kurejea katika enzi ya kidikteta
  • Wengi walikesha katika medani ya Tahrir kuelezea kero lao dhidi ya katiba mpya

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.