Yaliyojiri Afrika kwa picha

Imebadilishwa: 14 Januari, 2013 - Saa 08:06 GMT

Picha za Afrika wiki hii

 • Wacheza densi wakicheza katika mji mkuu wa Ghana Accra, kabla ya kuapishwa kwa rais John Mahama siku ya Jumatatu. Upinzani ulisusia sherehe hizo ukidai kuwa rais Mahama alishinda uchaguzi huo kwa wizi wa kura.
 • Huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa waumini walio wachache nchini Misri nchi inayoongozwa na waisilamu, wa Ethiopia ambao pia ni wakristo wa kopti wanahudhuria misa siku ya Jumamosi
 • Wanamitindo hawa wanatoa taswira ya ghasia zilizotokea katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati siku ya Jumatatu mjini Bangui. Wasanii na wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu waliandaa maonyesho yanye mada ya kuokoa nchi hiyo, ambayo imekumbwa na ghasia tangu Disemba.
 • Nyani hawa walipigwa picha wakijivinjari mitini mjini Durban Afrika Kusini
 • Mmiliki wa shamba la mizautini akipiga doria katika shamba lake lililoko katika mji wa Der Boorns . Eneo hili lenye viwanda vya thamani ya mabilioni ya dola vyenye kuzalisha mvinyo lilikumbwa na migomo ya wafanyakazi
 • Watoto mjini Abidjan, Ivory Coast, walivalia kupendeza wakimsubiri mkuu wa shirika la fedha duniani, Christine Lagarde. Katika ziara yake nchini humo, alisema kuwa uchumi wa nchi inayozalisha kakao kwa ukubwa duniani unaimarika hasa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwezi Aprili mwaka 2011
 • Vijana wapiga ngoma wa Burundi ambayo ni wahamiaji nchini Afrika Kusini, nao wakiukaribisha msimu wa kombe la taifa bingwa barani Afrika mjini Durban
 • Mashabiki wa soka nchini Afrika Kusini, wanashabikia timu ya taifa ya Bafana Bafana katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Norway mnamo Jumanne mjini Cape Town.Norway ilishinda kwa bao moja bila na kuzua wasiwasi kuhusu timu ambayo ndiye mwenyeji dimba la kombe la taifa bingwa Afrika litakaloanza tarehe 19.
 • Jamaa za watu waliouawa katika msongamano wa watu nchini Ivory Coast siku ya Jumatano. Maafisa walisema kuwa takriban watu 63 waliuawa kwenye msongamano huo mkesha wa mwaka mpya.
 • Mwanaume anatembea kando ya barabara iliyoharibika vibaya sana katika eneo la Reunion.Barabara hii iliharibiwa na kimbunga kilichipiga bahari hindi
 • Wanaume hapa wakipita kando ya mabaki ya lori lililoteketezwa nchini Nigeria kufuatia vurugu kati ya maafisa wa usalama na wanaume waliokuwa wanaiba mafuta

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.