Wabunge walivyopewa mazishi ya mzaha Kenya

Imebadilishwa: 18 Januari, 2013 - Saa 14:17 GMT

Wabunge Kenya wapewa mazishi ya kitaifa

  • Wanaharakati waliandamana kuafanya mazishi ya mzaha ya wabunge ambao walitaka kujizawadi mamilioni ya pessa za umma kama marupurupu yao mwishoni mwa muhula wao wa bunge
  • Katika baadhi ya mambo ambayo pia waliyataka ni mwananchi kugharamia mazishi ya wabunge watakapoaga kwa kuwafanyia mazishi ya kitaifa. Hata hivyo Rais Mwai Kibaki alikataa kutia saini mswaada ambao ikiwa ungeidhinishwa wabunge hao wangepokea mamilioni pamoja na mazishi ya kitaifa pindi wanapofariki
  • Na ndio sababu iliyochochea hasira ya wananchi waliofanya mazishi haya ya mzaha kuonyesha kero lao na kutaka kuwajulisha wabunge kuwa wamewazika katika makaburi ya sahabu kwa sababu ya ubinafsi wao
  • Waliandamana kupita mijini wakibeba mabango yaliyoonyesha kuwa wabunge wa Kenya ni wa binfasi
  • Wanaharakati waliwaita walafi na kuwafafanisha wabunge hao na ndege ambao hula mizoga ya wanyama
  • Hawakusita kuyachoma majeneza ambayo walikuwa wameyabeba mbele ya majengo ya bunge
  • Ishara ya hasira ya mlipa kodi wa Kenya kwa kuteketeza majeneza ya wabunge
  • Kwingineko wenyeji wa mji wa Garissa Kaskazini mwa Kenya walindama kuelezea kero lao kuhusu hali duni ya usalama
  • Walichoma magurudmu na kulaani serikali kwa kukosa kuwahakikishia ulinmzi wao. Hii ni baada ya siku ya Jumatano watu watano kuuawa na watu wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab
  • Wanataka serikali kuwahakikishia usalama wao

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.