Yaliyojiri Afrika kwa picha

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 14:42 GMT

Picha wiki hii

 • Wapenzi hawa wako kwenye mji wa bandarini wa Benghazi nchini Libya wakivinjari katika bahari ya Mediterranean huku meli zikipita katika upeo wa macho siku ya Jumapili.
 • Siku ya Ijumaa wanakijiji katika milima ya Atlas nchini Morocco wakisubiri chakula , magodoro na blanketi ambavyo vinatolewa kwao kama msaada kwa sababu ya msimu wa baridi kali.
 • Wanawake wakulima wanakusanya mchanga wa juu katika kijiji cha Djegbadji karibu na mji wa Ouidah nchini Benin. Baadaye watauchanganya na maji na kisha kuuchemsha na baadaye kupata chumvi ambayo wao huuza.
 • Mwanamume katika nchi jirani ya Nigeria, anatumia mtumbwi wake siku ya Jumapili kukimbilia usalama wake baada ya kutokea mlipuko uliosababishwa na watu waliokuwa wanajaribu kuiba mafuta. Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa angalau watu 3 walifariki.
 • Siku nne baadaye, wanajeshi kutoka Afrika Magharibi waliokwenda Mali kusaidia na harakati dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu, walionekana hapa kabla ya kuondoka kwao katika kituo cha wanajeshi wa kulinda amani mjini Kaduna Kaskazini mwa Nigeria.
 • Mjini Bamako, vijana wanacheza mpira wa miguu siku ya Jumanne siku tano baada ya mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Kiisilamu kaskazini mwa Mali waliokuwa wanasonga mbele kuelekea maeneo ya Kusini.
 • Siku ya Jumapili, raia wa Tunisia wajionea majina ya wale waliofariki katika mapinduzi ya kiraia dhidi ya serikali huku nchi hiyo ikijiandaa kwa sherehe za kuadhimisha miaka miwili baada ya kufanyika mapinduzi hayo.
 • Machifu katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanahudhuria sherehe mjini Kinshasa, kumkumbuka rais wa kwanza wa taifa hilo Patrice Lumumba, mnamo Alhamisi, miaka 42 tangu apigwe risasi
 • Naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta anawahutubia mashabiki wake mjini Nairobi, Jumamosi, alipozindua rasmi kampeini yake ya urais. Mgombea mwenza wake William Ruto, ambaye ni hasimu wake wa zamani wa kisiasa lakini wote wawili wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu wa kivita Hague.
 • Makurutu mjini Mogadishu wako kwenye shughuli ya mafunzo ya kuzima moto yaliyaondaliwa na jeshi la Muungano wa Afrika.
 • Wachimba migodi wa kampuni ya madini ya Anglo Platinum nchini Afrika Kusini, wakinong'onezana baada ya kazi , kampuni hiyo imesema inapanga kuwafuta kazi wafanyakazi 1,400
 • Mashabiki wa soka waking'ang'ania nafasi ya kumsalimia nyota wa soka Didier Drogba alipowasili katika uwanja wa ndege nchini Afrika Kusini kombe la mataifa ya Afrika yaliyoanza Jumamosi

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.