Mjadala wa kaunti ya Meru

Image caption Washiriki wa kipindi cha Meru

Kaunti ya Meru ina idadi ya wakazi milioni 1.3 kulingana na sensa ya 2009 wengi wao wakiwa ni wa jamii ya WaMeru.

Kaskazini mwa Meru ni kaunti ya Isiolo,

Mji wa Meru ni makao makuu ya kaunti hii.

Kaunti ya Meru inayashirikisha maeneo bunge 7 yakiwemo; Igembe, Ntonyiri, Tigania ya Magharibi, Tigania ya Mashariki, Imenti ya Kaskazini, Imenti ya Kati na Imenti ya Kusini.

Uti wa mgongo wa uchumi wa kaunti hii ni kilimo. Pamoja na kaunti jirani ya Tharaka, Meru imesifikasanana biashara ya miraa. Pia kahawa, majani chai na viazi hukuzwa katika eneo hili.

Hivi karibuni, serikali ya Uholanzi ilipiga marufuku uuzaji wa biashara ya miraa, hatua ambayo ilionekana kuwa kipigo kikubwa kwa uchumi wa kaunti ya Meru.

Sema Kenya ilizuru Kaunti ya Meru ili kuwapa wakazi wa eneo hili fursa ya kutoa hoja zao. Wakazi wapatao 100 na jopo la viongozi na wataalamu walijumuishwa kwenye mjadala huo kuzungumzia masuala hayo.

Miongoni mwa yale yaliyozungumziwa ni pamoja na suala la ukuzi na biashara ya miraa, ugavi wa ardhi na ufisadi.