Huwezi kusikiliza tena

Martha Karua. Kwa nini anagombea?

Martha Karua, mwanamke pekee anayegombea urais, anajiamini kuwa anaweza kushinda uchaguzi huu, baada ya kujitokeza kama mtu mwenye ari kutaka kushinda.

Hilo lilijitokeza katika mjadala wa wagombea wa urais uliofanyika Jumatatu jioni.

Alijitosa uwanjani na wagombea wengine wanane wakiwemo, Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

Na mwishoni aliweza kuwahakikishia wakenya kuwa wanaweza kumuamini.Karua alikuwa waziri aliyesifika kwa ujasiri wake kisiasa ingawa baadaye alijiuzulu kutoka kwa wadhifa huo. John Nene alizungumza naye kujua nini kinamshawishi kuwa anaweza kushinda uchaguzi.