Huwezi kusikiliza tena

Mfumo mpya na changamto zake

Kenya itakuwa na mfumo mpya wa serikali baada ya uchaguzi mkuu mwezi ujao. Kutakuwa na jumla ya kaunti 47 ambazo zitasimamiwa na magavana.

Wasiwasi wa Wakenya wengi ni kwamba huenda baadhi ya magavana hao wakafuja mali ya umma kama ilivyo kawaida nchini Kenya.

Lakini mwenyekiti wa mamlaka ya mpito nchini Kenya Kinuthia Wamwangi anasema wameziba kila njia ya ufujaji wa mali ya umma kwa hivyo magavana watalazimika kufuata sheria na njia ambazo wamewekewa wakitaka fedha.

John Nene amezungumza na Wamwangi kuhusu swala hilo nyeti.